Jarida la Emerging Infectious Diseases linasema kwamba zaidi ya magonjwa 200
yanaweza kusababishwa na chakula. Hata hivyo, vijidudu vinavyosababisha
magonjwa hayo yote si vingi sana.
Huenda
takwimu zifuatazo zinaweza kufanya mtu afikiri hivyo. Kulingana na Shirika la
Afya Ulimwenguni (WHO), kila mwaka watu milioni 130 hivi katika Eneo la WHO
huko Ulaya wanaambukizwa magonjwa yanayosababishwa na chakula.
Katika mwaka wa 1998, zaidi ya watu 100,000 nchini Uingereza
walikuwa wagonjwa kwa sababu ya kula chakula kibaya, na 200 kati yao walikufa.
Inakadiriwa kwamba kila mwaka watu milioni 76 hivi wanapata magonjwa
yanayosababishwa na chakula huko Marekani, na 325,000 kati yao hulazwa
hospitalini, na 5,000 hufa.
Si rahisi kujua hesabu kamili ya ulimwenguni pote. Hata hivyo,
shirika la WHO linaripoti kwamba watu milioni 2.2 hivi walikufa kutokana na
magonjwa ya kuharisha katika mwaka wa 1998, na milioni 1.8 kati yao walikuwa
watoto. Ripoti hiyo inasema: “Wengi kati ya wagonjwa hao waliambukizwa magonjwa
yanayosababishwa na chakula au maji machafu.”
Huenda ukashtuka kusikia takwimu hizo kubwa, Lakini je, takwimu
hizo zikufanye uwe na wasiwasi mwingi juu ya chakula? Bila shaka la. Ebu
fikiria mfano mwingine. Kila mwaka watu milioni 4.2 hivi nchini Australia wanapata
magonjwa yanayosababishwa na chakula, yaani watu 11,500 hivi kila siku! Huenda
hiyo ikaonekana kuwa idadi kubwa sana. Lakini kwa upande mwingine: Waaustralia
hula milo bilioni 20 kila mwaka, kwa hiyo ni milo
michache sana inayosababisha magonjwa.