Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Tuesday, January 5, 2016

WAZIRI WA AFYA UMMY MWALIMU AKAGUA KAMBI YA KIPINDUPINDU YA NYANKUMBU MKOANI GEITA

Wananchi wa Mkoa wa Geita wameaswa kufuata kanuni za usafi wa mazingira ili kudhibiti maumbukizi ya ugonjwa wa kipindupindu,Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu mara baada ya kutembelea kambi ya kipindupindu iliyopo kwenye kituo cha afya cha Nyankumbu,mkoani hapamli1
Waziri Ummy akivaa vifaa maalum vya kujikinga na kipindupindu kabla ya kuingia kwenye kambi hiyo,kulia ni Mganga mfawidhi wa Kituo hicho Josephat Msafiri.
(Picha Zote na Catherine Sungura WAMJW-GEITA)
mli2  
Waziri Ummy akivua vifaa hivyo mara baada ya kutoka kuwasalimia wagonjwa wa kipindupindu waliolazwa kwenye kambi hiyo,wagonjwa waliopo hadi leo mchana ni wagonjwa wanne

 
  mli3  
Waziri huyo akiongea na mmoja wa wagonjwa wa kipindupindu waliolazwa kwenye kambi hiyo mli4  
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akiwasalimia wagonjwa wa kipindupindu(hawapo pichani)kulia ni Mganga Mkuu wa Mkoa wa Geita Dkt.Joseph Kisala mli5 Baadhi ya wagonjwa wa kipindupindu waliolazwa kwenye kambi ya kituo cha afya cha Nyankumbu

No comments:

Post a Comment