Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Monday, February 15, 2016

HUZUNI:::MSANII WA BONGO FLAVOUR JOHN WOKA ALIPUKIWA NA MTUNGI WA GESI

MSANII anayejulikana kwa kurap kama mlevi, John Woka, amepata ajali ya kulipukiwa na mtungi wa gesi. Kwa sasa amelazwa kwenye hospitali ya taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam.
Walikuwa wanahangaika kurekebisha usafiri kwenye garage hapo Sinza, sasa katika kuhangaikia upande wa AC mtungi wa gas ukalipuka,moja ya vipande vya chuma chenye ncha kali kikamchoma kichwani. Madaktari wanahofia imefika mbali kiasi kwamba damu inamwagikia kwenye ubongo.


Mpaka hapa bado hajapata fahamu,mipango ya matibabu inaendelea. Tunasubiri kuambiwa kinachotakiwa kufanyika na mahitaji. Hospitali pale yupo kaka yake ambaye anapatikana kwa number ya Woka +255767007005 na mzee wake,kwa yoyote ambaye angependa kufika,kujua kinachoendelea au kuchangia chochote anaweza kumpigia tu moja kwa moja

No comments:

Post a Comment