Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Thursday, March 10, 2016

RAIS MAGUFULI AMKARIBISHA KATIKA DHIFA RAIS WA VIETNAM IKULU JIJINI DAR ES SALAAM.


 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli akizungumza na viongozi mbalimbali toka Tanzania na Vietnam kwenye halfa ya kumkaribisha Rais wa Jamhuri ya Kisoshalisti Mhe. Truong Tan Sang iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Kisoshalisti Mhe. Truong Tan Sang akizungumza na viongozi mbalimbali toka Tanzania na Vietnam katika halfa ya kumkaribisha  iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli akigonga glass na Rais wa Jamhuri ya Kisoshalisti Mhe. Truong Tan Sang ikiwa ni ishara ya ushirikiano kati ya Tanzania na Vietnam katika halfa ya kumkaribisha iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam.

 
 Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Jenerali Davis Mwamunyange (Wa pili kulia) akifatilia hotuba za Rais wa Tanzania na Vietnam katika halfa ya kumkaribisha iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam kulia ni Mkuu wa Jeshi la Polisi Inspekta Jenerali Ernest Mangu, wa pili kushoto ni Mkuu wa Jeshi la Magereza Kamishna Jenerali  Casmir Minja, katikati ni Mkuu wa Usalama Rashid Othman na kushoto ni Kamanda wa Kanda maaalum Dar es Salaam Kamishna Simon Sirro.
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi (katikati) akifatilia halfa ya kumkaribisha Rais wa Jamhuri ya Kisoshalisti Mhe. Truong Tan Sang iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam kushoto ni Naibu spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson na kulia ni Mnadhimu Mkuu mstaafu wa Jeshi la wananchi la Tanzania Luteni Jenerali Abdulrahman Shimbo.Picha zote na Raymond Mushumbusi MAELEZO.

No comments:

Post a Comment