Baada ya Mchungaji Gwaijima
kukanusha ripoti zilizotolewa na Polisi kwamba Mtuhumiwa wa kumtesa Dr
Ulimboka amekamatwa baada ya kutoa ushuhuda kanisani kwake, Kamanda wa
polisi kanda maalum ya Dar es salaam Suleiman Kova amesema jeshi la
polisi haliwezi kuingia kwenye malumbano na taasisi yoyote ya kidini
kuhusiana na kukamatwa kwa mtuhumiwa wa kwanza kwenye kesi ya kutekwa na
kuteswa kwa mwenyekiti wa jumuiya ya madaktari Dr Ulimboka Steven kwa
sababu ishu iko Mahakamani tayari.
Amesema taarifa zote zilizotolewa mwanzoni kuhusu Mtuhumiwa Getu Muhindi kwenda kwenye hilo Kanisa ni za kweli na uhakika.
Kova amesema daktari ndiye
mwenye mamlaka ya kuthibitisha kama mtuhumiwa ana matatizo ya akili au
ni mzima pamoja na kusisitiza kwamba ishu ya Dr Ulimboka isizungumziwe
popote kwa sababu iko Mahakamani.
“sasa halizungumziki nje ya
ulingo wa Mahakama, ukitaka kupata habari kuhusu shauri hili unakwenda
Mahakamani siku ya kutajwa lakini nje ya hapa mtu yeyote akifanya hivyo
anakiuka taratibu za katiba, mimi pia nafungwa mikono pamoja na kwamba
nafahamu mambo mengi na ningeweza kutoa ufafanuzi mwingi sana lakini
nimefungwa mikono yangu na utaratibu huo”


No comments:
Post a Comment