Waandamanaji wanaoipinga serikali wajilitokeza kwa wingi Jumatatu kumtaka waziri mkuu kujiuzu
Waziri mkuu wa Thailand Yingluck
Shinawatra ametangaza kwamba analivunja bunge na ataitisha uchaguzi wa
mapema , "kwa haraka iwezekanavyo" kufuatia maandamano ya zaidi ya mwezi
mmoja mjini Bankok kuipinga serikali yake.
Katika hotuba kwa taifa Jumatatu asubuhi kiongozi huyo alisema atawaachia wananchi kuamua mustakbal wa nchi yao.
Hata hivyo kiongozi wa chama cha upinzani cha Demokratic, Suthep Thaungsuban amesema hatositisha maandamano na wataendelea kuandamana hadi ofisi za Bi. Yingluck. Polisi waliripoti kwamba maelfu kwa maelfu ya watu waliandamana kuelekea makao makuu ya serikali siku ya Jumatatu asubuhi.
Wabunge wa upinzani walijiuzulu Jumapili na kusema hawawezi kufanya kazi na bunge linalopingwa na wananchi. wamesema ingawa ameitisha uchaguzi lakini hawatosita hadi Bi Yingluck ameacha madaraka.

No comments:
Post a Comment