Mikutano
ya IMF inaendelea, wakati huo huo mikutano mingine ikichukua nafasi
yake na kusaidia kujadili mambo ambayo yanaweza yakalisaidia Bara la
Afrika. Mawaziri wa Fedha wa Afrika wakiambatana na Magavana wao wa
Benki kuu leo wamehudhuria mkutano wa “CAUCUS”. Mikutano hii inafanyika
kwa lengo la kuwakutanisha Mawaziri wote wa Afrika ili kuweza
kuzungumzia matatizo yao kwa ujumla na wakisha yakamilisha huyachambua
na kuyapeleka kama ripoti moja kwa Rais wa Benki ya Dunia na kwa
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Fedha la Kimatafa.Katika kikao hicho,
Mawaziri hao wanazungumzia ni jinsi ni gani Taasisi hizo mbili
zinavyoweza kuzitoa Nchi za Afrika na ni maeneo gani ambayo Afrika
ikisaidiwa inaweza kuendelea.
Katika
picha juu ni Waziri wa Fedha Dkt. William Mgimwa akiwa pamoja na Gavana
wa Benki kuu Bw. Benno Ndulu kwenye mkutano wa Mawaziri wa Afrika
wakifuatilia mkutano wa Mawaziri wa Afrika ( Caucus meeting) ambapo
majadiliano hayohuafikiwa kwa pamoja na kupelekwa ngazi za juu za
uongozi wa IMF.Mkutano huo ulifanyika leo jijini Tokyo-Japan.
(Picha na Ingiahedi Mduma na Scola Malinga)
Mawaziri
wa Fedha wa Afrika katika mkutano wa pamoja wa Mawaziri Jijini Tokyo-
Japan,mkutano huo unajulikana kama (Caucus meeting).
No comments:
Post a Comment