Mkurugenzi
mtendaji wa NSSF Ramadhani Dau akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi
wa ofisi mpya ya mfuko huo katika eneo la Usa river Wilayani Arumeru
mkoani Arusha leo
Aliyevalia
suti nyeusi ni mkurugenzi mwendeshaji wa NSSF Cricentus Magori katikati
ni mkurugenzi mkuu Ramadhani Dau wakiingia katika eneo la uzinduzi leo
mjini Arumeru
Wadau
mbalimbali,wafanyakazi na wanachama wa NSSF wakiwa ndani ya jengo hilo
jipya ilikujionea namna ofisi zilivyokamilika tayari kwa huduma
Mfuko
wa hifadhi ya jamii (NSSF) imezindua ofisi mpya katika kata ya
Usariver wilayani Arumeru ikiwa ni moja kati ya kuboresha huduma za
wanachama wake katika wilaya hiyo ili kuweza kuwasogezea huduma
wananchi karibu zaidi.
Akizungumza
katika uzinduzi huo mkurugenzi mtendaji wa nssf bw. Ramadhani Dau
amesema kuwa wilaya hiyo ni moja kati ya wilaya ambazo zinaiingizia
michango mingi zaidi katuika mfuko huo ambapo amesema kuwa mwezi
huingiza milioni 432 kwa mwezi.
Bw.Dau
aliongeza kuwa mchango huo kwa mwezi ni mkubwa sana kwa kuwa ndani ya
mwaka mzima ni sawa na shilingi biloni tano hali mbayo inaashiria kuwa
kukiwa na ofisi hiyo karibu kutaongeza idadi ya wananchama wengine wapya
katika mfuko huo.
“mfuko
wa hifadhi ya jamii umeona ni vyema kama watatumia njia nzuri kuwa
karibu na wananchama wake kwa kuweka ofisi hii nyinyi ili kuwapunguzia
bughudha ya kufuatilia mafao pamoja na kuweka michango yenu hivyo
nadhani hii itawasidia sana”alisema bw.Dau
Aidha
alifafanua kuwa lengo la nssf kufungua ofisi hiyo ni ili kuwa karibu na
wananchama ili waweze kuweka michango yao kwa urahisi zaidi na
kuwapunguzia gharama za kufuatilia mafao wanachama ambapo ahapo awali
walikuwa wanalazimika kufuata huduma zote za mfuko mjini Arusha.
Kwa
upande wake Mkurugenzi wa uendeshaji bw.Cricentus Magori alisema kuwa
shughuli ambazo zinafanyika katika wilaya hiyo haswa mashamba makubwa
ya maua ambayo yapo maeneo mbalimbali,shughuli za uchimbaji wa madini
ndio chachu ya kupata michango mingi ,na wnachama wengi katika wilaya
ya arumeru.
Bw.Magori
alisema kuwa kwa sasa wilaya hiyo ina wanachama elfu saba ambapo
alisema kuwa wameona ni muhimu kufungua ofisi ili kuwapatia huduma na
kuondoa usumbufu wa kufuata huduma hizo mjini Arusha.
Katika
uzinguzi huo uliofana sana ulifanyika katika kata ya usa river
wilayanu arusmeru na kuwashirikisha wafanyakazi na wanachama wa mfuko
huo pamoja na wadau mbalimbali .
No comments:
Post a Comment