LADY JAYDEE
Mkurugenzi wa Machozi Band, Lady Jaydee akizungumza na
waandishi
wa habari jijini Dar es Salalaam leo wakati wa uzinduzi wa
kipindi chake
cha 'Diary Ya Lady Jaydee' kitakachoanza kurushwa hewani kila
siku ya Jumapili kupitia televisheni ya EATV. Kushoto ni Mkuu wa
Vipindi EATV, Lydia Igarabuza.
Mkuu wa vipindi wa Televisheni ya EATV, Lydia Karabuza akifafanua jambo wakati wa
uzinduzi wa kipindi cha televisheni cha 'Diary Ya Lady Jaydee
kitakachoanza kurushwa hewani kuanzia Jumapili.
DAR ES SALAAM, Tanzania
Msanii, Lady Jaydee amefanikiwa na kutambulika katika
kiwanda cha
muziki ndani na nje ya nchi, huku akitunukiwa tunzo nyingi
zaidi akiwa
albamu zake tano. Pamoja na kuwa anaendelea na fani yake ya
muziki, Lady Jaydee ameamua kuwafikia na kuwaburudisha
wapenzi wa kazi zake kwa njia nyingine.
Lady Jaydee sasa anaanza sura mpya ya burudani kwa kuleta kipindi
cha TV kiitwacho DIARY YA LADY JAYDEE, ambacho kutaonekana
katika kituo cha TV cha EATV
Diary Ya Lady Jaydee itaonesha maisha na hadithi za kweli za Lady
Jaydee kwa lengo la
Kuburudisha kwa kuonesha mambo yate mazuri anayopitia au
kuyaona Lady Jaydee
Kuelimisha kwa kushiriki mambo ya kijamii
Kutia moyo wengine wafuate ndoto zao kwa uadilifu
Kuongeza Kipato kama msanii kwa kutangaza biashara
mbalimbali na hatimae kudumisha ajira binafsi kwa
njia ya sanaa.
SHUKRANI
Lady Jaydee anatoa shukrani kwa mashabiki kwa kuendelea
kumpokea, jambo ambalo linampa nguvu zaidi ya kufanya kaza.
pia anashukuru sana vyombo vya habari na zaidi anawashukuru
EATV na washirika wake kwa kumpa nafasi ya kurusha kipndi
chake kipya Diary Ya Lady Jaydee.
EATV imekuwa mchango wa aina yake katika kuwakuza
wasanii Tanzania.
WITO
Lady Jaydee anatoa wito kwa vyombo vya habari kuendelea
kushirikiana na naye kwa kila namna, ili kukuza na kuendeleza
kipaji chake na sanaa ya muziki wa Tanzania kwa ujumla wake.
Zaidi anatoa wito kwa makampuni kishiriki na kuungana nae
ili waweze kumpa nguvu msanii, kutangaza biashara zao na
kushawishi ajira katika fani ya muziki.
Na mwisho Lady Jaydee anawaribisha wote kusikiliza CDs zake
au kuburidika na kundi lake la Machozi Band au kupata chakula
ktk mgahawa wake wa kisasa Nyumbani Lounge au ukiwa
umepumzika nyumbani utazame kipindi chake Diary Ya
Lady Jaydee ktk EATV

No comments:
Post a Comment