MWENYEKITI wa klabu ya Simba Alhaj Ismail Aden Rage
amesema kwamba uongozi umebaini kwamba wengi wa wanachama wa tawi la
Mpira Pesa waliojiorodhesha ili kushinikiza kufanyika kwa mkutano wa
dharura wa klabuu hiyo si hao.
Hatua
hiyo inafuatia wanachama hao kufanya maadhimio ya kujiorodhesha ili
kufikisha akidi itakayotimiza mashaerti ya kufanyika kwa mkutano ili
kuwaonmdoa madarakani viongozi wa sasa kwa madai ya kushindwa kuongoza.
Rage amesema pamoja na kubaini hilo,
pia uongozi umegundua kwamba majina ya wanachama hao yamenakiliwa
katika leja ya wanachama ambayo ilipotea mikononi mwa kiongozi mmoja wa
zamani.
Alisema
uongozi unaheshimu jitihada zinazofanywa na wanachama hao na kuzifanyia
kazi, lakini hauwezi kutekeleza vitu ambavyo havikidhi vigezo vilivyopo
katika katiba ya klabu hiyo.
Rage
alisema, katiba ya sasa ya Simba haiwatambui wanachama waliopo kwenye
leja, badala yake inawatambua wale waliosajiliwa katika kompyuta.
“Pamoja
na wanachama hao kunakiliwa katika leja,tumebaini hata saini zilizowekwa
ni za kughushi na tukifanya uchunguzi hasa tutabaini ni wengi tu hawana
sifa, kitu ambacho kinakwenda kinyume na katiba ya Simba,”alisema Rage
Rage
aliongeza kuwa, wanaamini mchakato huo unafanywa na baadhi ya watu
wanaotaka kuleta chokochoko ndani ya klabu hiyo kitu ambacho ni kigumu
kukitimiza kwa vile uongozi upo imara na unafuata katiba ya klabu hiyo.
“Hatuwezi
kujiuzuilu kwa ajili ya shinikizo la watu ambao tunafahamu wanatumika,
sisi tunaongoza kwa kufuata katiba na tutachukua uamuzi kwa mujibu wa
katiba pindi inapostahili,”alisema
Aidha,
Rage aliongeza kwamba uongozi wa klabu hiyo ulitarajiwa kukutana jioni
ya jana kwa ajili ya kujadili masuala mbalimbali ikiwemo mwenendo mbaya
wa timu hiyo katika mzunguko wa kwanza wa ligi kuu ya Vodacom
uliomalizika wiki iliyopita na Simba kushika nafasi ya tatu.
Hivi
karibuni baadhi ya wanachama waliutakla uongozsi wa Simba chini ya Rage
kuachia ngazi baada ya timu hiyo ambayo ilikuwa ikiongoza ligi kwa
kipindi kirefu kupoteza mwelekeo baada ya kupoteza michezo yake.

No comments:
Post a Comment