Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Friday, March 29, 2013

TASWIRA NA TAARIFA ZAIDI YA JENGO LA GOROFA LILILOPOROMOKA JIJINI DAR ES SALAAM ASUBUHI YA LEO



Kwa maelezo ya shuhuda, inasemekana limeanguka saa moja asubuhi ambapo kwa muda huo kulikua na watoto wa kihindi wanacheza mpira, kulikua na vibarua ambao wanataka kumwaga zege kuendelea na ujenzi na ndio walikua wanabadilisha nguo kuanza kazi.Ni posta mtaa wa Indira Gandhi pembeni ya msikiti mkubwa wa Itnasheri, lilikua ni gorofa la floor 12 ambapo mpaka sasa hakuna hesabu kamili ya vifo lakini shuhuda anasema kwa muda mfupi baada ya kuanguka alishuhusia maiti 12.
Mabaki ya jengo hilo lililoporomoka jijini da es salaam amablo lipo barabara ya morogoro mtaa wa indiana.

Wananchi waliokuwa eneo la tukio kwa ajili ya kusaidia kukoa wakijitahidi bila mafanikio kwa kuwa hapa ni lazima kuwepo na vifaa vya kunyanyua vitu vizito ili kurahisisha zowzi la kuokoa.

Bango la mmiliki wa jengo hilo mjenzi msimamizi wa jengo lililoporomoka leo asubuhi
Mabaki zaidi ya jengo hilo

No comments:

Post a Comment