Dar es Salaam.
Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Kata ya Majani ya Chai
iliyopo Kipawa jijini Dar es Salaam, wametajwa kujiingiza katika kashfa
ya ngono, kuvuta na kuuza bangi katika moja ya nyumba zinazozunguka
shule hiyo.
Hilo ni
tukio lingine jipya, kwani mwishoni mwa mwaka jana, kuliibuka matukio ya
ajabu kwa wanafunzi wa Shule ya Msingi, Ruaruke, Rufiji mkoani Pwani
ambao walielezwa kujihusisha na uvutaji bangi hata kukonyeza na kubaka
walimu wao.
Mkuu
wa Sekondari hiyo, Jasinta Assey alikiri na kusema kwamba vitendo vya
uvutaji bangi na biashara ya ukahaba kwa wanafunzi wake, vinachangiwa na
askari wa Kituo kidogo cha Stakishari ambao alidai wanachukua rushwa
kwa wauzaji wa bangi na nyumba bubu za wageni. Akizungumza jijini Dar es
Salaam jana, Mkuu wa Shule hiyo, Jasinta Assey alisema ni kawaida ya
polisi hao kwenda kwenye nyumba hizo kunakofanyika biashara hizo na
kuchukua rushwa badala ya kutatua tatizo.
No comments:
Post a Comment