Marehemu Martha Charles baada ya kuchinjwa shingoni na mume wake.
HUU
ni ukatili kwa 100%! Martha Charles (22), mkazi wa Nyahanga wilayani
hapa ambaye ni mtumishi wa Halmashauri ya Mji wa Kahama ameuawa kinyama
kwa kuchinjwa shingoni na mume wake
Kaimu
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Shinyanga, Afande Onesmo Lyanga alisema
tukio hilo lilitokea katikati ya wiki iliyopita ambapo pia alimtaja mume
anayedaiwa kutekeleza unyama huo kuwa ni Asack Nzolela (29),
mfanyabiashara wa bucha la nyama ya ng’ombe.
Afande
Lyanga alisema mtuhumiwa alimchinja mkewe wakiwa wamelala chumbani
kwenye nyumba ya wazazi wa mwanaume huyo na baada ya kufanya ukatili huo
alikimbia.
Habari za
uhakika zilizopatikana kutoka katika familia ya marehemu zilisema
chanzo cha mauaji hayo ni ugomvi wa kifamilia ambapo mtuhumiwa alianza
kwa kumlaumu mama yake mzazi kwa kitendo cha kumtafutia kazi mkewe
katika Halmashauri ya Mji wa Kahama wakati yeye alikuwa hataki mkewe
afanye kazi.
Habari
zilizopatikana eneo la tukio kutoka kwa mmoja wa ndugu anayeishi na
familia hiyo, Paul Edward alisema mbali na kuchinjwa shingoni pia
marehemu alikatwakatwa sehemu mbalimbali za mwili wake.
Edward
alisema usiku wa tukio akiwa amelala katika moja ya chumba ndani ya
nyumba hiyo, alisikia kelele za ugomvi kutoka kwenye chumba cha wanandoa
hao hali iliyomfanya apige kelele zilizowafikia majirani ambao walifika
kutoa msaada.
Akasema majirani hao sanjari na yeye walimkuta mtuhumiwa ameshamchinja mkewe kwa kisu na kutoweka kusikojulikana.
No comments:
Post a Comment