Muda mfupi uliopita spika wa bunge, Anna Makinda amelazimika kusitisha shughuli za bunge mwanzoni tu mwa hotuba ya kambi rasmi ya upinzani iliyokuwa ikisomwa na waziri kivuli wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Joseph Mbilinyi aka Sugu.Kauli kwenye hotuba hiyo
iliyobabisha spika wa bunge asitishe shughuli za leo hadi jioni ilisema, “Tanzania imegeuka chini ya usimamizi wa wizara ya serikali hii ya CCM kuwa taifa linalotoka nyara wanahabari, kuwatesa, kuwangoa kucha na meno, kuwatoboa macho, kuwamwagia tindikali na hata kuwaua.”
Spika amesitisha bunge hilo ili kupata muda wa kuipitia hotuba hiyo kuondoa kauli za uchochezi.
Sikiliza kipande hicho hapa.
Washindi Tuzo ya Kiswahili ya Safal kujulikana Ijumaa
-
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa ALAF Limited, Hawa Bayumi
(katikati) akitangaza orodha fupi ya waandishi waliofanikiwa kutinga
fainali ya T...
17 hours ago

No comments:
Post a Comment