Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Sunday, June 9, 2013

MBEYA CITY MOTO WAKE HAUZIMWI, WASUKA KIKOS MATATA CHA MAKINDA KUZISUMBUA TIMU ZA LIGI KUU MSIMU UJAO!!


488123_216997305113321_161758080_n
Ikiwa katika harakati za kujenga timu ya muda mrefu, klabu mpya ya ligi kuu soka Tanzania bara msimu ujao, Mbeya City ya jijini Mbeya anaendelea na mpango wake wa kuandaa kikosi cha pili cha klabu hiyo kwa lengo la kuwa na timu ya ushindani kitaifa na kimataifa.
Kocha msaidizi wa klabu hiyo inayonolewa na kocha Juma Mwambusi, Mwalimu Maka Mwalwisyi ameimabia FULLSHANGWE kuwa kwa sasa wanaendelea na mazozezi ya kikosi cha pili ambacho kimeteuliwa na benchi la ufundi la klabu hiyo, wakati viongozi wa timu  wakiweka mambo safi ili timu A iingeia kambini kujiandaa na michuano ya ligi kuu msimu ujao.
“Tunataka kuijenga falsafa ya Mbeya City, kufanikisha hilo tunahitaji kuwa na timu bora ya vijana ambao tutakuwa tunawapandisha timu A.  Kwasasa tupo na vijana wengi sana, tunajaribu kuchambua wanaotufaa ili kupata timu ya chini ya umri wa miaka 20”. Alisema Mwalwisyi.
Kocha huyo alisema kuwa wachezaji wao wanaonesha juhudi kubwa ya kujifunza, jambo ambalo linatia matumaini kwa benchi la ufundi.
“Vijana wana vipaji vya hali ya juu. Wanacheza kwa kujituma sana, mbali na hayo wana nidhamu ya mazoezi, wanazingatia sana maelekezo ya waalimu wao”. Alisema Mwalwisyi.
Mwalwisyi alisisitiza kuwa malengo yao ni kuifanya Mbeya City kuwa klabu ya ushindani mkubwa na sio washiriki wa ligi kuu bara.
Aidha alisema katika kuhakikisha hilo, benchi la ufundi linataka kuwekeza katika soka la vijana ambao ndio chagua sahihi kwa soka la sasa.
“Soka la kisasa kwa kweli linahitaji sana vijana ambao wanaenda sambamba na kasi ya mpira wa dunia, kwa kulijua hilo, Mbeya City lazima iwe kitalu cha kuzalisha wachezaji wa Tanzania”. Alisema Mwalwisyi.
Pia kocha huyo aliwataka mashabiki wa Mbeya kuwaunga mkono wao na ndugu zao Tanzania Prisons, wawakilishi wa jiji la Mbeya michuano ya ligi ya Premia ya Tanzania bara.
habari na fullshangwe blog

No comments:

Post a Comment