Mkuu wa wilaya ya Songea Joseph Mkirikiti akiongea kwa msisitizo ofisi juu ya mgogoro
ulijitokeza baina ya wachinja ng’ombe na wauzaji hapani ofisini kwake alipokuwa akiongea na waandishi wa habari
Aliyenyoosha kidole ni Issa Bakari akionyesha banda lililobomolewa na Afisa mifugo wa manispaa ya Songea
Hawa
ni wachinjaji wa ng’ombe wakiwemo wauzaji wa ng’ombe wakiwa katika hali
ya majonzi baada ya kuvunjiwa banda la kuhifadhia ng’ombe kabla ya
kuchinja
Waandishi
wa habari wakimuoji Afisa mifugo mkoa wa Ruvuma Bw. Mwaiganju
aliyesimama katikati ni mwandishi wa habari wa ITV Bw. Nathan Mtega ,
anaefuata ni mwandishi wa habari wa radio Jogoo Millan na alieshikilia
kamera ni Demasho
Hawa ni baadhi ya ng’ombe ambao wapo uwanjani baada ya kuvunjwa banda
………………………………………………….
MGOGORO
umeibuka baina ya wachinjaji na wauzaji wa ng’ombe wa Manispaa ya
Songea dhidi ya baadhi ya watumishi wa idara ya mifugo wa Manispaa ya
Songea mkoani Ruvuma ambao umesababisha wachinjaji na wauzaji wa ng’ombe
kuitisha mgomo usio na muda maalumu mpaka ufumbuzi wa tatizo hilo ambalo walidai ni la muda mrefu upatikane.
Mgogoro
huo ambao ulianza Juni 4 mwaka huu majira ya saa 12.30 jioni na kudumu
mpaka majira ya saa 2 usiku mwenyekiti wa umoja wa wachinjaji wa ng’ombe wa Mmkoa wa Ruvuma Salum Mfamaji ambaye pia ni diwani wa kata ya Misufini alipotangaza
kusitisha huduma hiyo mpaka hapo ufumbuzi wa tatizo hilo ambalo
lilikuwa liliwataka wachinjaji na wauzaji wa ng’ombe kuondoka katika
eneo hilo na kwenda kufanyia shughuli zao katika kata ya Tanga ambako
wao walidai hakujaandaaliwa.
Akizungumza
kwa niaba ya wachinjaji Issa Bakari alisema kuwa wao kama wachinjaji
hawajakaidi uamuzi wa Manispaa ya Songea kuhamia katika eneo hilo jipya
lakini walishaomba eneo hilo lifanyiwe marekebisho muhimu ikiw ni pamoja
na kuweka miundo mbinu muhimu ikiwemo vyoo na maji kwa
ajili ya usalama wa kiafya kwao na watu wengine watakaokwenda katika
eneo hilo kwa ajili ya kupata huduma hiyo muhimu.
Alisema
kuwa tangu kulipotokea mabadiliko ya watumishi katikas halmashauri ya
Manispaa ya Songea na hasa katika idara ya mifugo kumeibuka na vitendo
vya unyanyasaji kwa wachinjaji vinavyofanywa na baadhi ya watumishi wa
idara hiyo ikiwa ni pamoja na kitendo cha kuamua kuvunja zizi la
kuwafadhi ng’ombe kabla ya kuchinjwa kitendo ambacho kimefanywa bila
kutolewa taarifa kwa wachinjaji na wao wameamua kusitisha huduma hiyo
kwa jamii.
Baada ya mjadala wa muda mrefu diwani wa kata Msamala eneo ambalo machinjio
yapo Sharif Mgwasa alipowaomba wachinjaji hao kuendelea kutoa huduma
hiyo muhimu kwa jamii wakati uongozi ukiendelea na mazungumzo ya kutafua
ufumbuzi wa tatizo hilo lililojitokeza ikiwa ni pamoja na kujua
aliyeamuru kuvunjwa kwa zizi hilo bila kuzingatia utaratibu wa
ushirikishwaji wa wachinjaji’wauzaji na uongozi wa Manispaa hiyo.
Hata
hivyo wachinjaji hao waliendeleakusisitiza kuwa hawako tayari kuendelea
na huduma hiyo mpaka hapo ufumbuzi wa tatizo hilo utakapopatikana hali
iliyoendelea mpaka Juni 4 mwaka huu majira ya saa 2 asubuhi walipoamua
kuanza kuchinja ingawa ni ng’ombe wachache waliochinjwa kwa sababu ya
sintofahamu hiyo iliyotokea huku eneo hilo la machinjio likitawaliwa na
vurugu zilizosababisha askari polisi kufika eneo hilo na kutuliza ghasia
hizo.
Naye
Mkuu wa wilaya ya Songea Joseph Mkirikiti akizungumzia hali hiyo
iliyojitokeza alisema kuwa hiyo imetokana na kutokwepo kwa
ushirikishwaji wa pande zote zinazohusikia lakini pia suala la kuvunja
zizi hilo haliafiki ni si utaratibu wa busara kwa sababu ni kitendo cha
kihuni na hakipaswi kufumbiwa macho kwa sababu wachinjaji na wafugaji
walipaswa kuandaliwa mazingira mapya ya kufanyia shughuli zao na suala
la kuwahamisha lingefuata.
Hata
hivyo ufumbuzi wa sintofahamu hiyo unatarajiwa kufikiwa kesho kwa
kuzikutanisha pande zote kwenye ofisi ya Mstahiki Meya wa Manispaa ya
Songea
No comments:
Post a Comment