Mkurugenzi
wa Wananchi Progamming, Bi. Hannelie Bekker (katikati) akizungumza
na waandishi wa habari kuhusu maonesho ya filamu, utamaduni, kazi za
mikono na burudani yajulikanayo kama Zanzibar International Film
Festival (ZIFF) yanatarajiwa kufanyika mjini Zanzibar kuanzia tarehe 29
Juni hadi tarehe 7 Julai mwaka huu. Kulia ni Mkurugenzi wa Tamasha la
ZIFF, Profesa Martin Mhando na kushoto ni Mkuu wa masoko Wananchi
Programming Bi. Wangeci Murage. Picha na Maelezo.
………………………………………….
Na Genofeva Matemu na Lorietha Laurence – MAELEZO
MAONESHO
ya filamu, utamaduni, kazi za mikono na burudani yajulikanayo kama
Zanzibar International Film Festival (ZIFF) yanatarajiwa kufanyika mjini
Zanzibar kuanzia tarehe 29 Juni hadi tarehe 7 Julai mwaka huu.
Hayo yamesemwa
leo na Mkurugenzi wa Tamasha la ZIFF Profesa Martin Mhando alipokuwa
akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na tamasha hilo la 16 la
kimataifa litakalohusisha nchi za Jahazi jijini Dar es Salaam.
Alisema dhamira kuu ya tamasha hilo ni kuhakikisha kuwa ZIFF inaleta mabadiliko katika tasnia ya filamu hapa nchini kwani imekuwa ikitoa ajira za muda mfupi kwa washiriki wote na kuibua vipaji kwa kuzingatia kazi mbalimbali za sanaa na wasanii.
“Kupitia
tamasha hili la 16 tunatarajia kutoa ajira za muda mfupi kwa washiriki
wa filamu mbalimbali na kuibua vipaji kwani mara nyingi tumekuwa
tukifanikisha malengo ya wasanii mbalimbali na kuwawezesha kuwa wasanii
mahiri katika tasnia ya filamu” amesema Prof. Mhando.
Naye
Meneja Tamasha la ZIFF Bw. Daniel Nyalusi amesema kuwa tamasha
limewahusisha watayarishaji wa filamu zaidi ya 35 mahiri kutoka nchi
mbalimbali duniani ambao filamu zao zimechaguliwa kuingia ZIFF na kuwapa
fursa hiyo maalumu kuongelea filamu zao na utengenezaji wa filamu kwa
ujumla.
hapa
nchini kuhudhuria kwa wingi na kupata nafasi ya kubadilishana mawazo na
wenzao toka nchi mbalimbali ili kuweza kukuza vipaji vyao na kuweza
kutoa filamu nzuri zitakazonyanyua soko la filamu hapa nyumbani.
“Miaka
ya nyuma Tanzania hatukuwa na filamu nzuri katika soko la filamu hivyo
kusababisha filamu za kinaijeria kuchukua nafasi kubwa na kuwafanya
Watanzania wengi kufatilia filamu hizo ,lakini kwa kipindi hiki filamu
zetu zimekuwa zikija juu kwa kasi kubwa sana hivyo kuua soko la filamu
za kinaijeria kitu ambacho ni kizuri kwa taifa letu” amefafanua Bw.
Nyalusi.
Alisema katika
maandalizi ya tamasha hilo linalohusisha nchi za Jahazi ZIFF
lilihusisha filamu 257 toka nchi mbalimbali ambapo filamu 80
zilifanikiwa kuchaguliwa, kuoneshwa ili kuweza kushindania tuzo za ZIFF
za mwaka huu.
No comments:
Post a Comment