Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Tuesday, July 9, 2013

NDOTO YA USAIN BOLT KUICHEZEA MANCHESTER UNITED YAKAMILIKA - KUVAA JEZI YA MANCHESTER KWENYE MECHI YA HESHIMA YA RIO FERDINAND


Ndoto za mwanariadha Usain Bolt kuichezea Manchester United zinakaribia kuwa kweli - na hii ndoto itakamilika wakati wa mechi ya heshima ya Rio Ferdinand mwezi ujao.

Mwanadamu huyo mwenye kasi zaidi duniani atavaa jezi ya Man United kwenye mechi dhidi ya Seville katika dimba la Old Trafford.

Chanzo cha habari kilisema:“Usain hatimaye ametimiza ndoto yake na ataungana na wachezaji wengine kwenye mechi ya heshima ya Rio.

Mjamaica huyo, 26, huko nyuma alimuomba boss wa zamani wa Unitedpreviously Sir Alex Ferguson kumpa nafasi ya kufanya majaribio ya kuichezea United. Lakini mpaka kocha huyo anaondoka kwenye kiti cha umeneja Bolt hakuweza kupata nafasi ya kuichezea Unitd.

Lakini kutokana na urafiki uliopo baina ya Rio na Bolt, beki huyo wa kimataifa ameweza kumshawishi boss wake mpa David Moyes kumpa nafasi Bolt katika kikosi cha United kitakachocheza kwenye mechi yake ya heshima - baada ya kuitumikia klabu hiyo kwa takribani miaka 10.


No comments:

Post a Comment