BONDIA Ramadhani Kido wa jijini Dar es Salaam, Ijumaa iliyopita aliushangaza umati uliofurika kwenye Ukumbi wa Dar Live, Dar es Salaam baada ya kusema ameona jini mbele yake.
...Akiinuka baada ya konde hilo.
Kido alitoa kauli hiyo baada ya kutandikwa konde zito la kidevuni na mpinzani wake, Chupaki Chipindi wa Iringa.Katika pambano hilo lililokuwa la raundi sita, Kido alitandikwa
konde hilo katikati ya raundi ya kwanza na kuanguka mzimamzima ulingoni, kisha akainuka na kujaribu kuendelea lakini akashushiwa konde jingine kidevuni lililomlaza chini, hivyo kujikuta akipoteza pambano hilo kwa K’O katika raundi hiyo.
...Akiulizwa na mwamuzi kama ataendelea na pambano na kukubali.
Akizungumza na Championi Jumatatu baada ya pambano hilo, Kido alisema
kabla hajapigwa konde la kwanza lililomdondosha chini, aliona kitu cha
ajabu kama jini mbele yake, kisha akashtukia kishindo kizito kwenye taya
lake.
...akiwa chini tena baada ya kupokea konde lingine lililomaliza mchezo.
“Yaani hata sielewi ni kitu gani, nimeona kitu fulani kama jini mbele
yangu kimenipitia kwa kasi, kabla ya kusikia kishindo kizito kikitua
kwenye taya langu na kujikuta naanguka chini na kupoteza pambano,”
alisema Kido.
...akijaribu kuinuka kwa taabu.
Naye Chipindi baada ya kumtandika bondia huyo, alisema ukali wa ngumi
yake ndiyo uliomtia kiwewe bondia huyo na kuwaomba waandaji wa masumbwi
kumtafutia bondia mwingine wa kuzichapa naye.
...Baadhi ya wapambe wake wakiwa hawaamini kilichotokea.
Pambano hilo lilikuwa ni la utangulizi kabla ya mabondia wengine
Francis Miyeyusho wa hapa nchini na Darius Lipupa wa Zambia kuzichapa.
Miyeyusho alishinda kwa pointi.
No comments:
Post a Comment