Katibu Mkuu wa Chadema Dr Wilbroad Slaa akipungia mkono baada ya
kufika Uwanja wa Ndege wa Dulles nchini Mareani leo tarehe 21 Septemba
2013. Dr Slaa anatarajia kufanya mkutano na Wakazi wa Washington dc
tarehe 22 septemba 2013 katika Ukumbi wa Mirage uliopo University BLVD.
Pichani ni makamanda waliojitokeza Uwanja wa Ndege wa Dulles Kumpokea
Katibu mkuu wa Chadema Dr Wilbroad Slaa ambaye anatarajia kufanya
Mkutano na Watanzania wanaoishi Washington DC na maeneo mengine yaliyo
karibu.
Kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa Tawi la Chadema Washington DC (DMV)
Mh Kalley Pandukizi. Katibu Mkuu wa Chadema Dr Wilbroad Slaa, Mke wa
Katibu mkuu Mama Josephine Mushumbuzi na Katibu wa Tawi na Afisa wa
Habari wa Chadema DMV Mh Liberatus Mwang'ombe
Dr Slaa akipeana Mkono na Mwenyekiti wa Tawi la Chadema Washington DC
(DMV) Mh Kalley Pandukizi mara baada ya Dr Slaa kufika Marekani kwa
ziara ya siku kadhaa.
Dr Slaa akipeana Mkono na Katibu wa Tawi na Afisa wa Habari wa Tawi
la Chadema Washington DC (DMV) Mh Liberatus Mwang'ombe mara baada ya Dr
Slaa kufika Marekani.
Katibu Mkuu wa Chadema Dr Wilbroad Slaa akipeana mkono na Katibu wa
Baraza la wanawake Bi Baybe Mgaza uwanja wa ndege wa Dulles alipowasili
akitokea Tanzania.
Katibu Mkuu wa Chadema Dr Wilbroad Slaa Akipena mkono na Katibu wa
Baraza la wazee Mh Elias Mshana uwanja wa ndege wa Dulles Marekani.
Katibu Mkuu wa Chadema Dr Wilbroad Slaa akipeana mkono na Mweka
Hazina wa Tawi la Chadema Washington DC (DMV) Mh Ludigo Mhagama kwenye
uwanja wa Ndege wa Dulles nchini Marekani.
Katibu Mkuu wa Chadema Dr Wilbroad Slaa Akiwa na watoto wa Mbunge wa
Viti maalum wa Chadema Kwimba Mh Leticia Nyerere, Julia Nyerere
(Kushoto) na Helena Nyerere (Kulia).
No comments:
Post a Comment