MWENYEKITI
wa Klabu ya Simba, Ismail Aden Rage, amemtaka Mkuu wa Mkoa wa Dar es
Salaam, Mecky Sadick kuhakikisha anawahamisha watani zao Yanga katika
eneo la Jangwani kwa kuwa ni hatarishi kwa maisha yao.
Akizungumza
wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Nani Mtani Jembe jijini Dar es Salaam
jana, Rage mbali ya kumsifu Sadick kwa kuwaondoa baadhi ya watu na
kuwapeleka Mabwepande, anamuomba awaondoe na Yanga kwani ni eneo
hatarishi kwa maisha yao.
Alisema,
yeye kama mtani wa Yanga, hahitaji kuwapoteza watani zake, hivyo basi
anamuomba ahakikishe anawaondoa katika eneo hilo kama alivyofanya kwa
watu wengine.
"Mimi
nitahakikisha napeleka muswada huo bungeni, kwani wale wengine walitoka,
hivyo basi namuomba Mkuu wa Mkoa awaondoe na Yanga eneo hilo kwani ni
hatarishi pia kama walivyoondolewa wengine," alisema Rage ambaye pia ni
Mbunge wa Tabora Mjini na kuwavunja mbavu mashabiki wa Yanga waliokuwepo
katika eneo hilo.
Wakati
Rage akimtaka Sadick kufanya hivyo, wiki iliyopita mkuu huyo wa mkoa
aliwaruhusu Yanga kuwahamisha watu waliovamia eneo lao kwa kuwa
walishawaondoa siku nyingi toka kipindi cha mafuriko, huku Manispaa ya
Ilala ikiwataka kukagua mipaka na kujiridhisha kwanza.
No comments:
Post a Comment