Sehemu ya
wafanyakazi wa Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA),
wakimsikiliza Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe (hayupo pichani
wakati wa uzinduzi wa vichwa vipya sita vya treni vya Shirika hilo, leo
asubuhi katika stesheni ya TAZARA. Vichwa hivyo sita vimetolewa na
Serikali ya China.
Waziri
wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe akitoa hotuba wakati wa uzinduzi wa
Vichwa vipya sita vya treni vya Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia
(TAZARA), katika stesheni ya TAZARA leo Asubuhi. Kushoto kwa Waziri
Mwakyembe ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dk. Shaaban Mwinjaka.
Waziri wa
Uchukuzi wa Zambia, Yamfwa Mukanga, akitoa hotuba yake kwa wafanyakazi
wa Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA) kabla ya kuzindua
vichwa vipya sita, katika stesheni ya TAZARA leo asubuhi.
Waziri wa
Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe (kushoto), Muwakilishi wa Balozi wa
China nchini Tanzania,Bw. Li Xuhang (katikati) na Waziri wa Uchukuzi wa
Zambia, Yamfwa Mukanga(kulia), wakikata utepe kuashiria uzinduzi wa
vichwa vipya sita vya Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia(TAZARA)
vilivyotolewa na Serikali ya China, leo asubuhi katika stesheni ya
TAZARA.
Waziri wa
Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe (katikati), muwakilishi wa Balozi wa
China nchini Tanzania, Bw. Li Xuhang (wa tatu kutoka kwa Waziri
Mwakyembe) na Waziri wa Uchukuzi wa Zambia, Yamfwa Mukanga (katikati),
wakipeperusha bendera kuashiria kuanza kwa safari kwa vichwa vipya sita
vilivyozinduliwa leo katika stehseni ya TAZARA.
Waziri wa
Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe, akifurahia jambo na Wazazi wa Waziri
wa Mambo ya Ndani, Bw. Na Bi. John Nchimbi, wakati wa uzinduzi wa vichwa
sita vipya vya Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA),
vilivyozinduliwa leo Asubuhi, katia stesheni ya TAZARA
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Uchukuzi)
No comments:
Post a Comment