Katika
hali ya kuonyesha CCM hapako shwari leo mkuu wa Wilaya Gabriel Kimolo
amevua gamba na kuvaa Gwanda hii leo ni kwenye Kongamano linaloendelea
muda huu katika hotel ya Land mark ambapo wangeni rasmi ni Tundu Lisu,
Mnyika, Lema, Msigwa, Heche na Kilewo.
Akiongea
na watanzania waliojana kwenye kongamano hilo Kimolo amesema CCM
inakufa na kuna kila ishara za CCM kufa mfano kuuwa waandishi wa habari,
kutesa wana harakati, kutumia nguvu nyingi kuzoofisha upinza hasa
CHADEMA pia amewaomba watanzania kujiunga na chadema kwani kwasasa ni
tumaini la watanzania na kuna kila ishara kuwa inaenda kuongoza nchi...
Kwa
mujibu wa Bw. Kimolo, miongoni mwa sababu za kujiuzulu kwake ni pamoja
na kitendo cha yeye kukashifiwa na baadhi ya wafanyibiashara wanunuzi wa
kahawa Wilayani hapo, ambao walifikia hatua ya kumtamkia kuwa hawawezi
kuongea na "mbwa, bali na mfuga mbwa", wakimaanisha hawawezi kuongea
naye bali Waziri Maghembe ambaye inadaiwa alikuwa akiwakumbatia.
“Nimechoshwa
na kejeli na mizengwe dhidi ya serikali. Wafanyibiashara wanadiriki
kusema kuwa hawako tayari kuzungumza na mbwa bali wanazungumza na mwenye
mbwa. Siwezi kufanya kazi katika mazingira ya aina hii. Wananchi
waelewe hivyo. Nitabakia kuwa raia mwema na mwananchi wa kawaida kama
wengine” alisema Bw. Kimolo.
Kimolo,
ambaye anakuwa kiongozi wa kwanza wa Wilaya kuachia ngazi katika
kipindi cha miaka 20, ya utawala wa CCM, amesema kuwa amekuwa akikosa
Ushirikiano na Wizara ya Kilimo kwa ujumla juu ya msimamo wake wa
kupinga ununuzi wa kahawa mbivu (Red Cherry), kama ambavyo imekuwa
ikifanywa na baadhi ya wafanyibiashara wanaopata ridhaa toka Wizarani.
Januari
7 mwaka huu, Waziri Maghembe, alikutana na baadhi ya wakulima na wadau
wa zao la kahawa ambapo msimamo wa Serikali ulieleza kuwa hawako tayari
kuendelea kuwaona wakulima wakiuza kahawa mbichi kwa wachuuzi hao hali
ambayo Bw. Kimolo amesema ilisababisha yeye kuonekana kutothaminiwa
msimamo wake na Serikali ya Wilaya na ya Mkoa.
Kadhalika
katika maelezo yake ya kujiuzulu, amesema kuwa kwa mujibu wa utaratibu
wa uteuzi unaofanywa na Rais, yeye uteuzi wake ulianza mwaka 2006, na
kukoma mwaka 2010 ambapo hadi sasa hakuna uteuzi mpya uliofanywa na Rais
jambo ambalo linamfanya ashindwe kupanga mikakati ya kazi kwa maendeleo
ya Wilaya yake.
Amesema
kuwa, hivi sasa ni mwaka mmoja na nusu amekuwa akifanya kazi kwa
matukio ya dharura na maagizo toka juu na hivyo kumfanya aonekane
kutowajibika vilivyo katika nafasi yake na kwamba ameamua kujiuzulu
akiamini kuwa uamuzi wake utalinda heshima yake.
Aidha,
inaelezwa kuwa Bw. Kimolo amekuwa ni mtu wa karibu sana na Mbunge wa
Monduli, Edward Lowassa na kwamba kitendo chake cha kujiuzulu kina
baraka kutoka kwa kiongozi huyo aliyewahi kuwa Waziri Mkuu kablda ya
kujiuzulu, ambapo katika ziara yake aliyoifanya hivi karibuni Wilayani
Momba katika mji mdogo wa Tunduma, aliteta naye jambo muhimu.
Hata
hivyo, tetesi za kutokuwemo katika uteuzi ujao zinaelezwa kuwa ni moja
ya sababu zinazomfanya mkuu huyi kuachia ngazi mapema ili kujijengea
mazingira ya maandalizi ya kuikubali hali hiyo kabla haijatokea wakati
wa uteuzi ambao unatarajiwa kufanywa na Rais wakati wowote kuanzia sasa.
Akasema
kumekuwa na baadhi ya viongozi wababaishaji na kusababisha serikali
ionekane inashindwa kuwatumikia vyema wananchi na sasa yeye ameamua
kuachia ngazi na anakwenda kushughulika na mambo yake binafsi.
Alipotakiwa
kueleza kama dhamira yake imejikita zaidi katika siasa, amesema kuwa
wakati ukifika kuingia katika mchakato wa kisiasa atafanya hivyo kwakuwa
yeye kama mtu yeyote ana uamuzi wake na katiba inamruhusu kufanya
hivyo.
Amesema
kuwa, tayari amemuandikia barua Rais, Waziri Mkuu na Mkuu wa Mkoa wa
Mbeya kuwajulisha hilo na kwamba huo ni uamuzi wake binafsi na jibu
lolote halitabadili uamuzi wake huo.
No comments:
Post a Comment