Brandts
ambaye yupo katika kuitumikia notisi ya siku 30 aliyopewa na uongozi wa
Yanga ikiwa ni mpango wa kumuondoa katika cheo chake hicho.
KOCHA
Mkuu wa Yanga Ernie Brandts, amegoma kuendelea na kazi kama
alivyokubaliana na uongozi huku akisisitiza kwamba ana kikao na uongozi
kuweka sawa baadhi ya mambo.
Brandts
ambaye yupo katika kuitumikia notisi ya siku 30 aliyopewa na uongozi wa
Yanga ikiwa ni mpango wa kumuondoa katika cheo chake hicho, alishindwa
kuibuka katika mazoezi ya kikosi hicho, yaliyoendelea jana Ijumaa
asubuhi kwenye Uwanja wa Bora, Kijitonyama, Dar es Salaam akimuachia
msaidizi wake, Fred Minziro.
Habari
ambazo Mwanaspoti, imezipata baada ya Brandts kutoonekana katika
mazoezi hayo, zinadai kwamba kocha huyo alishindwa kutekeleza kwa
vitendo kuendelea kukifundisha kikosi hicho, badala yake amekuwa akitaka
kukutana na mabosi wa timu hiyo, kujadiliana nao jambo moja muhimu.
Imeelezwa
kuwa Brandts, ameona hataweza kuendelea kukifundisha kikosi hicho,
baada ya kubaini kuwa kuendelea kukifundisha kikosi hicho ndani a siku
30, hakutakuwa na maana tena kutokana na tayari viongozi wa Yanga,
wameonyesha nia ya kumuondoa huku wakianza taratibu mchakato wa kumsaka
mrithi wake, ikiwa ni kufikia mwisho kwa utawala wa Mholanzi huyo
aliyedumu kwa msimu mmoja na nusu.
Habari
zinasema Brandts alipanga kukutana na Makamu Mwenyekiti wa Yanga,
Clement Sanga jana jioni kumalizana naye ili asiendelee na majukumu yake
kwa vile ameona hayatakuwa na tija katika kikosi hicho.
Brandts
alipoulizwa alisema: “Nimeshindwa kuja mazoezini, hicho ndicho
ninachoweza kukwambia kwa sasa, sitaki kuongea nawe kwa kirefu naomba
uelewe hilo, nasubiri leo(jana) jioni naweza kukutana na uongozi kuna
jambo nataka kujadiliana nao.”
CHANZO: MWANASPOTI
No comments:
Post a Comment