Mashirika
ya kutoa misaada, yalitozwa pesa na wanamgambo wa Al Shabaab ili yaweze
kuruhusiwa kuingia katika maeneo waliyokuwa wameyadhibiti, wakati wa
janga la njaa mwaka 2011.
Taarifa hii ni kwa mujibu wa taasisi mbili za utafiti barani Afrika.
Hata
hivyo wakati mwingi, al-Shabab ilisisitiza kusambaza chakula wenyewe na
wakati mwingine hata kukichua badala ya kuwapa watu waliokuwa
wanakumbwa na njaa.
Baadhi ya
mashirika hayo yangali yanalipa Al Shabaab ili yaruhusiwe kuingi katika
maeneo ambayo watu wanahitaji msaada nchini Somalia na hasa maeneo
ambayo bado kundi hilo linadhibiti.
Zaidi ya watu 250,000 walifariki wakati wa janga hilo mwaka 2011.
Ripoti
hiyo iliyotolewa na taasisi ya kimataifa ya maendeleo na ustawi pamoja
na taasisi nyingine ya sera mjini Mogadishu, ilitaja pesa hizo kama
malipo ya usajili na mashirika hutozwa hadi dola 10,000 za kimarekani.
Taasisi
hizo zinasema kuwa wakati mwingine al-Shabab ilichukua chakula
kilichonuiwa kupelekewa watu kama msaada katika mji wa Baidoa
No comments:
Post a Comment