Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiweka jiwe la msingi
la Jengo jipya la Skuli ya Maandalizi ya Kikosi cha 14 cha Ali Khamis
cha JWTZ Vitongoji Chake chake Pemba.
Nyuma ya Balozi Seif ni Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba akiwa pia Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Mh. Dadi Faki Dadi.
Mkuu wa
Kikosi cha 14 Kambi ya Ali Khamis Vitongoji Chake chake Pemba Luteni
Kanali Julius Khombwe Mbwero akimpatia maelezo ya ujenzi wa Majengo ya
Skuli ya Ali Khamis Kamp Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif
Ali Iddi aliyetembelea majengo hayo mara baada ya kuweko jiwe la msingi
ya jengo jipya la skuli ya Maandalizi ya skuli hiyo.
Kushoto yake ni Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba Dadi Faki Dadi na Mkuu wa Wilaya ya Chake chake Bibi Mwanajuma Majid.
Makamu wa
Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akimpongeza Rais wa Serikali ya
Wanafunzi wa Skuli ya Kambi ya Ali Khamis Vitongoji Ridhiwan Khalfan
Hamad mara baada ya kumwaga kimombo { Kiiingereza } wakati akiwasilisha
Risala ya wanafunzi hao.
Balozi
Seif akiikagua Hospitali ya Jeshi la Ulinzi wa Tanzania { JWTZ }
ya Kikosi cha 14 Viongoji Pemba mara baada ya kuweka jiwe la msingi la
Skuli ya Kikosi hicho.
Picha
no:- 105 ni:- Balozi Seif akiuahidi Uongozi wa Kikosi cha 14 Vitongoji
kwamba Serikali ya SMZ itajipanga kusaidia baadhi ya vifaa,
watendaji hospitali hiyo ili itoe huduma bora zaidi.
Makamu wa
Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akiagana na Mkuu wa Kikosi cha 14
cha Ali Khamis Vitongoji Chake chake Pemba baada ya kuweka jiwe la
msingi la skuli ya maandalizi ya kikosi hicho pamoja na kutembelea
Hospitali yaKambi hiyo.
Picha na Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ.
Uwamuzi
wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania { JWTZ } Kikosi cha 14 cha Ali Khamis
kiliopo Vitongoji Chake chake Kisiwani Pemba wa kuanzisha Skuli ya
Maandalizi, Msingi na hatimae melekeo wa Sekondari umesaidia kuunga
mkono azma ya Serikali kupitia Sera ya Elimu ya kulenga kuwapatia Elimiu
ya lazima watoto wote wa Taifa hili.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alieleza hayo mara
baada ya kuweka jiwe la msingi la Jengo Jipya la Skuli ya Maandalizi ya
Ali Khamis Camp iliyoanzishwa na Makamanda na wapiganaji wa Kikosi hicho
cha 14 Vitongoji hafla ambayo ilipata Baraka pia na wazazi na wanafunzi
wa Skuli hiyo.
Balozi
Seif alisema jamii inafahamu juhudi kubwa zinazoendelea kuchukuliwa na
Jeshi la Wananchi wa Tanzania { JWTZ } katika kusaidia masuala ya
Kijamii katika wakati wa amani jambo ambao huleta faraja kwa wananchi
wanaozizunguuka kambi za Jeshi hilo katika maeneo mbali mbali Nchini.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar alikipongeza Kikosi hicho cha 14 cha Ali
Khamis kiliopo Vitongoji Chake Chake Pemba chini ya usimamizi wa Mkuu wa
Kikosi hicho ambae ndie muanzilishi wa Skuli Hiyo Luteni Kanali Julius
Khombwe Mbwelo kwa wazo lao la kufikiria kuanzisha skuli hiyo.
Balozi
Seif alisema uwamuzi huo umekuja katika kipindi muwafaka utakaochangia
kwa kiasi kikubwa kupunguza msongamano wa wanafunzi kwenye skuli za
Serikali zinazozizunguuka Kambi hiyo.
Alielezea
faraja na kuvutiwa na uamuzi wa kizalendo wa Jeshi hilo wa kukubali
kuwapokea watoto wa raia wa jirani na Kambi hiyo ambao ni wa kupigiwa
mfano na Serikali Kuu inaangalia mazingira ya kuisaidia Skuli hiyo
ambayo kwa mazingira yake inahesabika kama ni skuli ya umma licha ya
kwamba inahudumiwa kwa nguvu za wanajeshi wenyewe.
“
JWTZ linafahamika kwa kuanzisha miradi mbali mbali inayosaidia jamii
katika maeneo tofauti Nchini ikiwemo Skuli za msingi na Sekondari, Vituo
vya Afya na hata kazi za kujitolea “. Alifafanua Balozi Seif.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliwataka wazazi na walezi wa wanafunzi
wanaosoma kwenye skuli hiyo kuhakikisha kwamba wanatoa ada zao ndogo
walizopangiwa kwa wakati ili huduma za wanafunzi zinazotolewa skulini
hapo ziendelee kama kawaida.
Katika
kuunga mkono juhudi za Makambanda na wapiganaji wakambi hiyo ya 14
Vitongoji Chake Chake Pemba Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi
Seif aliahidi kushirikiana na Shirika la Umeme Zanzibar katika
kuhakikisha Skuli hiyo inaondokana na tatizo la huduma za Umeme.
Balozi
Seif pia aliahidi kuchangia gharama za matofali elfu moja
yatakayosaidia kuendeleza ujenzi wa jengo aliloliwekea jiwe la nsingi la
Skuli ya Maandalizi pamoja na kusaidia mipira kumi ya mchezo wa soka na
kumi ya mchezo wa Pete.
Akitoa
Taarifa fupi ya Skuli ya Kikosi cha 14 cha Ali Khamis Mwalimu Mkuu wa
Skuli hiyo mwalimu Yugin Lutagengwa alisema skuli hiyo ilianzishwa
mwaka 2009 ikiwa na wanafunzi 39 na sasa wamefikia 604 wengi wao wakia
raia wa jirani wanayoizunguuka skuli hiyo.
Mwalimu
Yugin Lutagengwa alisema lengo la kuanzishwa kwa skuli hiyo chini ya
Mkuu wa Kikosi hicho Luteni Kanali Juius Khombwe Mbwelo ni kushiriki kwa
wanajensi katika Jamii wakati wa amani pamoja na kupunguza maafa kwa
watoto hasa pale wanapofuata elimu masafa ya mbali.
Hata
hivyo Mwalimu Mkuu Yugin alizitaja baadhi ya changamoto zinazoikabili
skuli hiyo kuwa ni pamoja na jamii kutoelewa elimu ya ushindani, uhaba
wa majengo kutokana na kuongezeka kwa idadi ya wanafunzi pamoja na
tatizo la huduma za umeme.
Katika
Risala yao iliyosomwa na Rais wa Serikali ya Wanafunzi wa Skuli hiyo
Mwanafunzi Ridhiwan Khalfan Hamad wameelezea kufarajika kwa kiwango cha
elimu wanachokipata katika skuli yao.
Hata
hivyo wanafunzi hao waliiomba Serikali na wafadhili kufikiria wazo la
kuwapatia huduma za mitandao Kompyuta ambayo wanaimani kwamba itaongeza
nguvu zao za ufahamu katika masomo yao mbali mbali.
Mapema
Kamanda wa Kikoci cha 14 cha Ali Khamis kiliopo Vitongoji Chake chake
Pemba Luteni Kanali Julius Khombwe Mbwelo alisema katika kuwajengea
mazingira bora ya kufaulu vyema wanafunzi wao Uongozi wa Skuli hiyo uko
katika juhudi za kujenga Bwalo la wanafunzi ili kuwapa utulivu katika
masomo yao.
Kamanda
Julius alisema hatua hiyo imelenga kuwaanda vizuri wanafunzi wa darasa
la saba walioingia mwaka huu ambao wanatarajiwa kufanya mtihani wa Taifa
kwa ajili ya kujiwekea malengo ya kuingia skuli za Sekondari za
Mchepuo.
Wakati
huo huo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif alikagua
Hospitali ya Jeshi hilo iliyopo jirani na eneo hilo ambayo pia hutoa
huduma za afya kwa askari pamoja na wananchi wanaolizunguuka eneo hilo.
Hospitali
hiyo kubwa imefanyiwa matengenezo makubwa kwa msaada wa Serikali ya
marekani ambapo baadaye inatarajiwa kuongeza huduma zake za afya
likiwemo suala la kulaza wagonjwa.
Mganga
Mkuu wa Hospitali hiyo Kepteni Said Omar Mwege alimueleza Makamu wa
Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif change moto wanazokabiliana nazo
kubwa likiwa ongezeko la wagonjwa ambapo uwezo wa kuwapatia huduma za
dawa ni mdogo.
Kepteni
Said alieleza kwamba licha ya mashirikiano mazuri yaliyopo kati ya
Uongozi wa Kambi hiyo na Uongozi wa Wizara ya Afya Pemba lakini suala la
upatikanaji wa dawa Hospitalini hapo linahitaji kuungwa mkono ya
Serikali.
Akitoa
shukrani zake Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif aliueleza
uongozi wa Hospitali hiyo kwamba Serikali itaangalia nama ya kuiwezesha
Hospitali hiyo kuendelea kutoa huduma kwa ufanisi.
Balozi
Seif aliuagiza Uongozi wa Hospitali hiyo kupitia Mkuu wa Kambi hiyo
kuorodhesha mapungufu yote yaliyomo ndani ya Hospitali hiyo ikiwemo
wafanyakazi ili Serikali ijipange katika kuona inatoa msukumo kwa
Hospitali hiyo.
Aliopungeza
Uongizo wa Kambi hiyo katika juhudi za kuimarisha huduma za afya kwa
uwamuzi wake wa Kujenga jengo jipya la huduma za uchunguzi wa X Ray,Utra
sound pamoja na ushauri nasaha kwa wananchi walioambukizwa na virusi
vya Ukimwi.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar balozi Seif Ali Iddi aliueleza Uongozi wa
Hospitali hiyo kwamba yeye binafsi ataangalia mazingira ya kusaidia
vitanda vya wagonjwa kwa ajili ya Hospitali hiyo katika kipindi kifupi
kijacho.
Credit: Zanzinews
No comments:
Post a Comment