Aliyekuwa Rais wa Misri, Mohamed
Morsi, ameonyesha ukaidi katika siku yake ya kwanza katika mahakama
nchini Misri, kujibu tuhuma za njama ya kuwatorosha wafungwa kutoka jela
wakati wa mapinduzi ya kiraia ya Hosni Mubarak 2011
Morsi aliyefikishwa mahakamani na washitakiwa
wenzake, alihoji uhalali wa mahakama hiyo na kusisitiza kuwa yeye bado
ni rais halali wa nchi hiyo.Zaidi ya washitakiwa wengine 130 wakiwemo viongozi wa vuguvugu la Muslim Brotherhood wameshitakiwa pamoja na Morsi.
Bwana Morsi hajakuwa huru tangia jeshi limuondoe madarakani mwaka mmoja baada ya kuchaguliwa kama rais.
Wakati huohuo, wizara ya mambo ya ndani imesema kuwa afisaa mmoja wa wizara hiyo Generali Mohammed Saeed, alipigwa risasi akielekea kazini.
Mauaji hayo yanatokea wakati mashambulizi dhidi ya maafisa wa usalama katika siku za hivi karibuni na masaa kadhaa baada ya jeshi kumuunga mkono mkuu wake Field Marshal Abdul Fattah al-Sisi kugombea urais.
Hali ya usalama imeimarishwa nje ya ya jengo la wizara hiyo , lakini hakuna hata mfuasi mmoja wa Mohammed Morsi amejitokeza.
Vuguvugu la Muslim Brotherhood, limeharamishwa na kutajwa kama kundi la kigaidi na pia wameifanya hatia uungwaji mkono wa kundi hilo.
Makabiliano kati ya wafuasi wa Brotherhood pamoja na vikosi vya usalama, yaliripotiwa kutokea katika eneo la Ramses mjini Cairo.
Morsi anatuhumiwa kwa kosa la kupanga njama ya kuwatorosha wafungwa kutoka katika gereza la Wadi al-Natrun wakati wa ghasia za mwaka 2011.
Mara ya kwanza alipofikishwa mahakamani mwezi Novemba, Morsi alikataa kutambua uhalali wa mahakama wala kuvalia vazi la gerezani
No comments:
Post a Comment