Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Wednesday, March 5, 2014

KAULI KUMI(10) NA ZA KUSISIMUA ZILIZOVUTA HISIA ZA WENGI KWENYE BUNGE LA KATIBA MJINI DODOMA,ZISOME HAPA

Ni vigumu kueleza matukio yote yaliyotawala kauli na hisia za wengi kwa wiki nzima mjini Dodoma bila kuangalia  michango ya baadhi ya wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba.
Michango hiyo ya mawazo katika mjadala kuhusu rasimu ya kanuni zinazopaswa kuongoza kikao kwa siku 70 za kikao hicho, baadhi yake zilikuwa kali. 
Zifuatazo ni baadhi ya kauli hizo:

 1. Mchungaji Christopher Mtikila

Mtikila, ambaye ni mwenyekiti wa Democratic Party (DP), alitumia dakika tano kutoa somo kwa wajumbe wa Bunge hilo kuhusu umuhimu wa kupiga kura ya siri badala ya ile ya wazi.
Anasema haki ya kupiga kura kwa siri haitofautiani na haki ya mtu kuwa na miguu miwili na kwamba itashangaza akitokea mtawala akaamuru kila mtu awe na mguu mmoja, halafu watu wakakaa kujadili.
“Wote tutaonekana tuna matatizo ya akili,” alisema Mch. Mtikila.
Alisema Bunge Maalumu la Katiba litaingia katika hatia na aibu kwa kujadili mambo ya msingi ya kidemokrasia ambayo pia yameainishwa katika katiba ya sasa, likiwamo suala hilo la kura ya siri.
“Mwenyekiti (akimlenga Pandu Ameir Kificho) tumekuchagua kwa kura ya siri siyo kwamba tulikuwa wajinga kuliko wenzetu, hapana! Ni ‘democratic civility’ (ustaarabu wa kidemokrasia),” alisema.
 “Ni aibu waheshimiwa na hii nasema si jambo la mjadala kuna vitu vya kujadili, lakini si haki ya kupiga kura kwa siri. Hii ni haki ya msingi ya kidemokrasia,” alisema.

 2. Profesa Ibrahim Lipumba (Mwenyekiti –CUF Taifa)
Mwenyekiti huyo wa CUF alisema msingi wa kupiga kura ya siri ni kujaribu kuwalinda wajumbe ambao wanaweza kupiga kura kinyume na misimamo ya vyama vyao au makundi yao.
 Akijenga msingi wa hoja yake, Profesa Lipumba alisema hata Jaji Joseph Warioba katika taarifa yake alisema moja ya taasisi zilizotoa maoni ni Baraza la Wawakilishi lililopendekeza Serikali tatu.
“Tunadai kura za siri kusudi kuwalinda hawa wenzetu ambao wametoa misimamo, wakija kupiga kura hapa  inaweza kuwapa matatizo huko walikotoka,” alisema.
 Aliongeza : “Tunapolishabikia hili kuwa pasiwe na kura ya siri inaonekana wazi pana ajenda ya kuwashughulikia watakaokwenda kinyume cha msimamo.”

ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI 



 3. Esther Bulaya (Viti Maalumu-CCM)
Bulaya, tofuti na wajumbe wenzake wengi kutoka chama tawala (CCM), alionekana kutoa mchango uliogusa hisia za wengi hasa pale alipoeleza bayana kuwa hayuko tayari kuona ukandamizaji unafanyika kumlazimisha apige kura ya wazi.
Akirejea msimamo wa kura ya wazi unaoshabikiwa na wajumbe wengi wanaotokana na chama chake, alisema hawezi kupiga kura ya aina hiyo wakati anajua inamnyima uhuru wake.
“Nitasema kweli daima, fitina kwangu mwiko. Ni lini na wapi katika uamuzi mgumu kama huu kulifanyika kura za wazi kama wengi wanavyotaka,” alisema.

  4. Pandu Ameir Kificho (Mwenyekiti wa Muda)

Naye Kificho, ambaye pia ni Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, alionyesha kukerwa na baadhi ya vyombo vya habari hasa vilipolishikia bango suala la posho.
 “Kusema kweli, jamii tunaichanganya mpaka  jambo hili la kutupatia Katiba Mpya lionekane ni la mchezo au tumekuja kudai posho. Nawataka wenzetu (wanahabari) wawe makini sana juu ya jambo hili wasiupotoshe umma ili kazi hii isiingie dosari,” alisema.
Vyombo vyote vya habari vizingatie kupata habari kwa uwazi na ukweli kutoka kwa wanaohusika ili jamii yetu ya Watanzania ipate habari za kweli na hilo la kupokea tu posho kwa kusoma magazeti tunalikanusha kwa nguvu zote”.

 5. Philemon Ndesamburo (Moshi Mjini-Chadema)
Ndesamburo aliwataka wajumbe wenzake kuacha ushabiki wa kisiasa na kutambua wanatengeneza katiba itakayodumu miaka 50 ama miaka 10 ijayo.
“Tusilete ushabiki. Nawaombeni sana tusilete ushabiki katika jambo hili. Hili ni jambo zito. Hili ni jambo tunalolifanya kwa niaba ya Watanzania milioni 45 na sisi tumepata bahati tu; ni Mungu ametusaidia,” alisema.

 6. Profesa Jumanne Maghembe (Waziri wa Maji)
Profesa Maghembe alifananisha upigaji wa kura kwa siri  kuwa sawa na ule uliofanyika nchini Marekani wakati wa kashfa ya ufuska iliyokuwa ikimkabili aliyekuwa rais wakati huo, Bill Clinton.
“Kule Marekani walikuwa wakipiga kura ya kumwondoa madarakani Clinton kwa madai ya kushikwa ugoni. Walipiga kura ya wazi kwa sababu lilikuwa jambo kubwa la kumwondoa mtu madarakani,” alisema.
 Profesa Maghembe, ambaye pia ni Waziri wa Maji, aliwasihi wajumbe kutofautisha upigaji kura wa mwenyekiti wa kijiji, diwani, mbunge na rais ambao alisema wananchi hupiga kura za siri.
“Humu ndani tunatafuta sheria mama ya nchi. Tumepewa jukumu hilo kwa niaba ya Watanzania wote. Wao watapata nafasi ya kusema ndiyo au hapana. Sasa tunajificha ili iweje, tunamficha nani?” alihoji.
7. Sheikh Hemed Jengo
Sheikh Jongo alishauri Bunge Maalumu la Katiba kuwapa nafasi wajumbe wanawake watakaokuwa katika hedhi, waruhusiwe kuapa bila kushika kitabu kitukufu, Quran.
“Siku nyingine kinamama wanakuwa katika siku maalumu (hedhi). Ni haramu kwa mujibu wa dini kushika msahafu. Atakapojieleza kuwa hali yangu si nzuri, basi aruhusiwe kuapa hivyo hivyo kwa heshima,” alisema na kuongeza:
“Hata kwa wanaume wa Kiislaamu wakitaka kuapa wachukue udhu kwa sababu kitabu chenyewe kinakataza kukishika bila ya udhu. Ndiyo yamini. Ndiyo maana watu wengine hatuoni wanafanya vizuri kule nje kwa sababu wanajua waliapa bila udhu na haikuwa yamini.”

 8. Maria Sarungi Tshehai
Mwanaharakati huyo alitumia fursa aliyopewa kuwaponda wajumbe wenzake waliokwenda katika Bunge hilo kwa ajili ya kuwasilisha masilahi ya vyama.
“Hatuko hapa kwa ajili ya kuwasilisha vikundi mbalimbali. Tukianza hivyo itakuwa ni hatari sana katika Bunge hili,” alisema.
“Nianze kwamba kitu kilichonifanya nitoke nje nilifutwa (na mtu ambaye hakumtaja jina). Aliniambia wewe mbona unaonekana upo kwenye upande wa chama fulani.” 

9.Richard Ndassa (Mbunge wa Sumve)
Yeye alionekana kukerwa na baadhi ya taarifa za vyombo vya habari kuhusu suala la posho na kuvishtaki vyombo hivyo kwa mwenyekiti wa muda wa Bunge hilo, Pandu Ameir Kificho.
 “Wabunge wanachota milioni 129 kwa kikao cha dakika 30” na kingine kikisomeka, “Wabunge walipwa milioni 130 kwa dakika 25; Bunge la Katiba vipande vipande; wapewa posho kwa kusoma magazeti,” alisema akikariri vichwa vya habari vya baadhi ya magazeti na kudai vinamkera.

10. Dk. Zainab Gama
Naye mwanasiasa mkongwe, Dk. Zainabu Gama alikwenda mbali na kudai kuwa baadhi ya wanaotaka kura ya siri wametumwa na watu ama wamekula rushwa ndiyo maana hawataki kupiga kura ya wazi.
“Hatukuletwa hapa kimchezo mchezo.  Simama, sema mimi uamuzi  wangu huu kila mmoja akuone,” alisema.
MWANANCHI

TASWIRA ZA ENEO LA MWENGE JIJINI DAR LEO BAADA YA MVUA KUBWA KUNYESHA

 Mama akiwa anashangaa jinsi ya kupita eneo la karibu na maghorofa ya jeshi mwenge,huku mwingine akimamua kuyavaa maji bila kujali .
 Eneo la mtaa wa umoja street likiwa limejaa maji kutokana na mvua zilizonyesha leo jijini dar
 Maji yakiwa yamezuia kabisa eneo la mtaa wa umoja mwenge kutokana na  mvua kubwa zilizonyesha jijini dar.
 Mtaro ukiwa umezidiwa na maji,na kupelekea kuja mpaka barabarani.PICHA NA DJ SEK BLOG





TAZAMA PICHA ZA MZUNGU TAPELI ALIYEKAMATWA



 Mzungu aliyekuwa anatafutwa na Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kwa kutuhuma za kuwatapeli wananchi kwa Euro Feki hatimae amekamtwa kikomandoo akijaribu kununua gari kwa pesa hizo feki. 
 
Habari za uhakika zilizotua mezani zilisema mzungu huyo ambae ni Raia wa South Africa aliyeahamika kwa jina la  JAN ELOFF ambae anaishi maeneo ya Msasani Jijini Dar.


Kwa mujibu wa taarifa zilizonaswa na mtandao huu hatari kwa habari za uchunguzi zilisema mzungu huyo ambae alikuwa anatuhumiwa kumpiga zaidi ya Euro hizo feki 700 mwandishi mwandamizi wa blog hii na DTV Bw. Livingstone Mkoi mwanzoni mwa januari mwaka huu kisha kufungua kituo cha polisi Oysterbay nakupatia kumbukumbu hii OB/RB/ 2972/14 KUJIPATIA PESA KWA NJIA YA UDANGANYIFU,pamoja na Kutoa Euro Feki.

 

Baada ya tukio hilo la kutapeliwa mwanahabari huyo Jeshi la Polisi lilitangaza msako mkali wa kumtafuta mzungu huyo ambae alikuwa akishirikiana na wadada wawili ambao ni araia wa Cameroon na Nigeria pamoja na mwanaume wa kitanzania ambao baada ya tukio la kukatwa mwenzao wanaendelea kutafutwa usiku na mchana na tayari ameshawataja wenzake anaoshirikiana nao.ananchi wengi wamempongeza Kamanda Kova kwa kufanikisha kukamatwa mzungu huyo.

Hata hivyo Jeshi la Polisi Kinondoni limetoa rai kwa mtu yeyote ambae amewahi kupigwa na mzungu huyo basi wafike haaka kituo cha polisi Oysterbay kwa ajili ya kumtambua mzungu huyo..Imeandaliwa na
Livingstone Mkoi

KWELI KIPAJI HAKIZEEKI WATAZAME ZIDANE NA RONALDO DE LIMA WAKIONYESHA UMAHIRI WAO KWENYE MECHI YA HISANI

Football legends Zinedine Zidane and Ronaldo once again invited an all-star cast of former footballers to take part in their annual Match against Poverty.

With the event now in its 11th year, Zidane and Ronaldo were joined by the likes of Fernando Hierro, Paolo Maldini, Pavel Nedved and Luis Figo.
Taking on Young Boys in Bern, the former France star's side eventually went on to win 8-6, thanks to a double from the man himself.

Stars: An all-star cast of former players played in the 11th Match against Poverty - how many can you name?
Stars: An all-star cast of former players played in the 11th Match against Poverty - how many can you name?

Master: Zidane scored twice in an 8-6 victory over a Young Boys Bern XI
Master: Zidane scored twice in an 8-6 victory over a Young Boys Bern XI

Skipper: Ronaldo has a strike at goal Skipper: Ronaldo has a strike at goa

Mrisho Ngassa amzungumzia Amiss Tambwe wa Simba – hiki ndicho alichosema

DSC_1384


Kwa mara nyingine tena katika kipindi cha wiki mbili, winga machachari wa klabu ya Yanga Mrisho Khalfan Ngassa amemsifia mshambuliaji wa timu mahasimu Simba Mburundi Amiss Tambwe.

NGASSATAMBWE copy

Akitumia akaunti yake ya mtandao wa kijamii wa Twitter Mrisho Ngassa alimsifia Tambwe kwa kumuita mshambuliaji bora. Hatua hiyo ya Ngassa ilikuja baada ya Tambwe kufunga mabao mawili katika mchezo wa jana dhidi ya Ruvu Shooting uliopigwa uwanja wa taifa na Simba kutoka na ushindi wa 3-2.

UBOVU WA CHEMBA ZA KUPITISHA MAJI MACHAFU NJE YA HOSPITALI YA PALESTINA(SINZA) WAPELEKEA MAFURIKO NDANI YA HOSPITALI JIONEE


 Huu ni mtaro wa kupitisha maji taka ambao umepita kati kati ya Hospitali ya Palestina amapo ulifumuka na kusababisha kusambaa kwa maji machafu katika kila kona ya Hospitali hiyo
 Mmoja wa wagonjwa akiwa anangojea kupata huduma baada ya mvua hiyo kubwa kwisha
 Haya ni maji machafu ambayo yametapakaa kila sehemu ya hospitali
 Kushoto ni Mgonjwa akiwa amelala juu ya Benchi ambapo pembeni kuna maji na matope ambayo yamechanganyikana na kinyesi kutoka katika vyoo mbalimbali katika makazi ya watu.
 Hii ndio hali halisi ya Chemba hii ambayo ipo ndani ya Hospitali ya  Sinza Palestina
 Hizi ni chemba zaidi ambazo zipo nje na pia zimeungana na zilizopo ndani ya Hospital hiyo
 Wagonjwa zaidi wakingojea waganga kufika pia kumalizia kusafishwa kwa vyumba hivyo ili wapate hudumiwa
 Moja ya Chumba ambacho kilikuwa kimejaa tope kikingojea kusafishwa
 Hapa hata hapapitiki
 Baadhi ya viti vikiwa vimeegeshwa kwa ajili ya kungoja kufanya usafi
 Hakuna mtu katika maeneo haya kutokana na mvua kubwa iliyonyesha

 Kila kitu kimekaa hovyo hovyo baada ya mvua kubwa hiyo kunyesha
 Baadhi ya vifaa vya kutibia wagonjwa vikiwa juu ya moja ya kitanda cha kutibia wagonjwa huku watu wakingoja huduma ya matibabu.
 Huu ndio Mtaro wa maji machafu ambao hupitisha maji,lakini wakati wa mvua kubwa ukishindwa kupokea maji yanaingia ndani ya Hospitali
Picha zote na Dar es salaam yetu

MWANAMKE AJIFUNGUA NDANI YA BASI MBEYA


 Katika hali isiyokuwa ya kawaida mwanamke mmoja jina halijafahamika anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 20-25 akiwa na mumewe, wakitokea wilayani Chunya mkoani Mbeya
wakielekea wilayani Mbozi amejifungulia kwenye gari aina ya Coaster jana lenye namba T 653 CTC.
Gari hiyo ilikuwa ikielekea Tunduma ambapo imeelezwa kuwa Mwanamke huyo alijifungua mtoto wa kiume.
 
Mwandishi wa habari hii Moses Ngwa't anasema licha ya yeye kuwa shuhuda wa uzazi huo kwasababu alikaa na mjamzito huyo, Bibi mmoja ndye alikuwa shujaa wa kumzalisha binti huyo.

ALIYEUA BAADA YA KUMFUMANIA MKEWE AHUKUMIWA JELA MWAKA 1,KWA KUUA BILA KUKUSUDIA HUKO TABORA


Kijana Sanane Machimi akiwa mahakama ya hakimu mkazi mfawidhi mkoa wa Tabora  muda mfupi baada ya kuhukumiwa kifungo cha mwaka mmoja kufuatia kosa la mauaji ya bila kukusudia.Mahakama ya hakimu  mkazi  mfawidhi mkoa wa Tabora  imemuhukumu  kutumikia kifungo cha mwaka mmoja Jela  kijana anayefahamika kwa  jina la  Sanane Machimi baada ya kupatikana  na  hatia ya kuua bila kukusudia.

Akisoma  maelezo ya kosa mbele  ya mahakama hiyo,Mwanasheria upande wa Jamhuri  Bw.Nestory  Paschal  aliieleza mahakama hiyo kuwa mshtakiwa  Sanane Machimi akiwa na umri wa miaka  17 mnamo  tarehe  7 mwezi wa 5 mwaka  2012 alimuua bila kukusudia  mtu  mmoja aliyefahamika kwa jina la Kweji  Ntuvilo kwa kumpiga kwa fimbo kichwani na ubavuni  baada ya kumfumania  anafanya  mapenzi na mkewe  eneo la  vichakani  huko wilayani  Sikonge.

Mshtakiwa  alikiri  kutenda  kosa  hilo   kinyume na kifungu  namba  195 kanuni ya adhabu  sura  namba 16  marejeo  ya  sheria ya  mwaka  2002 ambapo  alieleza kuwa  baada  ya  kumkuta  marehemu  akifanya tendo  la  zinaa na  mkewe  haikuwa  rahisi  kwake  kuvumilia  kitendo  hicho na hivyo  kushikwa  na  ghadhabu  ya kumshambulia  hali iliyosababisha kifo cha marehemu  Kweji  Ntuvilo aliyekuwa na umri wa miaka 30.

Akisoma  hukumu   baada  ya  kusikiliza  maelezo ya pande zote mbili, hakimu mkazi  mwandamizi  mwenye mamlaka ya ziada Bw.Thomas  Simba  alisema mahakama hiyo  tukufu  imepitia kwa makini shitaka hilo na kumtia hatiani  Sanane  Machimi ambapo alimhukumu kutumikia kifungo cha kwenda Jela  kwa muda wa mwaka mmoja ili iwe fundisho kwa mtu mwingine atakayediriki kufanya kosa kama hilo.

Hata hivyo  mshtakiwa  mara  baada  ya  kusomewa  adhabu  hiyo  alisikika akimshukuru  Mwenyezimungu  akidai kuwa  adhabu  aliyoipata imekuwa na nafuu  sana kwake  kwakuwa  tayari  alikuwa  amekaa  mahabusu  tangu  mnamo  mwaka  2012. 
Credit-kapipij blog

CHAMA CHA MAPINDUZI CHASITISHA KAMPENI ZA UBUNGE KALENGA

Chama  Cha Mapinduzi (CCM) kilichokuwa kikifanya kampeni katika kijiji cha Kidamale Jimbo la Kalenga, kimelazimika kusitisha kampeni zake kwa muda ili kushiriki maziko ya watu watatu waliofariki dunia katika ajali ya gari iliyotokea katika jimbo hilo.
Ajali hiyo ilitokea juzi kwa kuhusisha gari la kiwanda cha kusambaza maji ya Afrika cha mkoani humu aina ya Isuzu Foward lenye namba za usajili T 750 AFJ. Aidha, ajali hiyo pia ilisababisha watu wanne kujeruhiwa. Waliokufa katika ajali hiyo ni Nyagile Luvanda (38), Sabasaba Kunzugala (35) na Anskali Chengula (20), wote wakazi wa kijiji cha Kidamali.
Majeruhi ni Shukuru Msigwa (20), Riziki Kyando (30), Jimmy Luvanda (21) na Spedito Mgongolwa (28), wote wakazi wa kiojiji cha Kidamali. Majeruhi hao walipelekwa katika hospitali ya Tosamaganga kwa matibabu.
 Akiongoza maziko hayo juzi, Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara), Mwigulu Nchemba, alisema CCM imepokea msiba huo kwa masikitiko makubwa na ndiyo maana wamelazimika kusitisha kampeni hizo na kushiriki kwenye maziko.

 Nchemba kwa niaba ya CCM alitoa Shilingi milioni moja kwa familia za marehemu hao huku Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), tawi la Kidamali, waklitoa Sh. 50,000. Miili ya marehemu hao ilizikwa katika makaburi ya kijiji cha Kidamali.
Aidha, Nchemba alisema kuwa endapo CCM itapewa ridhaa ya kuongoza katika jimbo hilo, mgombea wao  Godfrey Mgimwa, atasaidia watoto walioachwa na marehemu William Mgimwa.

MADIWANI 23 MERU WATAKA KUJIUZULU

picture2bno-2b2Na Gladness Mushi, Meru



BARAZA la madiwani Meru lenye jumla ya madiwani 23 limeathimia kujiuzulu nyadhifa hiyo ya udiwani endapo kama Serikali haitaweza kuingia kati masakata mbalimbali ya migogoro ya radhi iliyodumu kwenye halmashauri hiyo kwa muda mrefu
Uamuzi huo uliwekwa hadharani juzi mara baada ya kumalizika kwa baraza la madiwani lililofanyika katika halmashauri ambapo lilitoa siku chache kwa serikali kuweza kuingilia kati.
Akiongelea sakata hilo mmoja wa madiwani wa Halmashauri hiyo loti Nnko alisema kuwa sakata la migogoro ya ardhi kwenye halmashauri hiyo limedumu kwa muda mrefu sasa ndio maana wwamefikia uamuzi wa kutaka kujiengua katika nyadhifa hiyo ya udiwani.
Nnko alisema wanachokisubira kwa sasa ni majibu kutoka kwa kamati ambayo wameiunda ambapo kamati hiyo itaenda Jijini Dar es saalam wiki ijayo na watakaporudi basi watarudi na majibu ambayo yataweza kuwafanya kuondoka kwenye viti hivyo vya udiwani.
Akitolea mfano moja yashamba lenye migogoro katika Halmashauri hiyo,shamba la  Madira lililopo katika maeneo ya Seela Singisi ambalo  ni mali halisi ya Halmasahuri hiyo lakini kwa sasa kuna migogoro ambayo inasababishwa na baadhi ya viongozi jambo ambalo wamedai kuwa hawataweza kuvumilia bali wataingia katika vita kwa mara nyingine
“kwa mfano hili shamba la Seela Singisi ni mali ya wananchi wote wa Meru na hadi Raisi ameshaweka saini yake jamani litumike kwa ajili ya matumizi ya kata zote za Meru lakini vigogo wanasema ni mali yao alafu bado tumenyamaza tu haitawezekana tunaachia udiwani alafu htunaingia katika Vita kwa mara nyingine”aliongeza Kimu.
“hili ni tamko rasmi tunatoa tunataka majibu ya migogoro hii rasmi kama hatupewi itakuwa ni vita baina ya Wameru na hawa wanaojichukulia ardhi kinyemelea, pia itakuwa ni huzuni kubwa kwa CCM  manake kwanza sisi wote hapa tunatokea CCM uzalendo umetushinda kabisa”aliongeza Nyiti
Naye Mwenyekiti wa Halmasahuri hiyo ya Meru, Goodson Majola alisema kuwa tamko hilo la kutaka kujiuzulu kwa madiwani 23 wote wa halmashauri hiyo lipo sawa kabisa kwa kuwa migogoro yote ya ardhi inasababishwa na Viongozi wasio waadilifu kuanzia ngazi ya Halmashauri hadi Wizara
“mimi nasema kuwa tutajiuzulu wiki chache zinazokuja baada ya kujiridhisha juu ya maangaiko haya ya ardhi ambayo yamedumu toka karne hadi karne na ninasiistiza kuwa itakuwa ni kilio kwa CCM kwa kuwa wanchama wetu nao tutaweka chini ya ulinzi hadi tutakapowaambia hawatajishugulisha na shuguli yoyote ya chama”alisema Majola.
Majola alisema kuwa kujiuzulu kwao lakini pia kuondoka na wanachama wote wa CCM katika Wilaya hiyo ni uzalendo wao kwa wananchi na hivyo Hata CCM nao hawapaswi kuumia kwa hilo

RAIS KIKWETE AKUTANA NA WAZIRI WA BIASHARA WA UFARANSA

D92A3170D92A3149D92A3168Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Waziri wa Bishara na Mjumbe Maalumu wa Rais wa Ufaransa Mhe. Nicole Bricq ikulu jijini Dar es Salaam leo asubuhi.Mjumbe huyo aliwasilisha ujumbe huo wa Rais wa Ufaransa Francois Hollande na kufanya mazungumzo na Rais Kikwete(picha na Freddy Maro)


WATU WATATU WAPOTEZA MAISHA IRINGA

Watu watatu wafariki dunia katika matukio tofautitofauti mkoani Iringa likiwemo la Perizi Matiku (28) kujinyonga baada ya kutuhumiwa kuiba fedha kiasi cha shilingi 150,000/=.

Akizungumza na mtandao huu wa www.matukiodaima.com ofisini kwake leo Kamanda wa polisi mkoani Iringa Ramadhani Mungi alithibitisha kutokea kwa tukio hilo lililotokea mnamo tarehe 2 machi majira ya saa 9 kamili mchana katika kijiji cha Ikungwe, tarafa ya Kiponzero wilaya ya Iringa Vijijini.

Kamanda alisema marehemu alijinyonga kwa kutumia kamba iliyokuwa kwenye nguo huku chanzo kikiwa ni baada ya marehemu kutuhumiwa kuiba kiasi cha fedha za Juma Kapona.

Tukio lingine mtu mmoja aliyefahamika kwa jina Benard Muyemba (24) dereva wa IT amefariki dunia baada ya kuligonga gari kubwa aina ya scania.

Kamanda alithibitisha kutokea kwa tukio hilo lililotokea mnamo tarehe 2 machi katika barabara kuu ya Iringa- Njombe na  kusema marehemu alikuwa akiendesha gari aina ya Mistubishi Canter yenye namba za usajili It.4113 ambapo alimgonga kwa nyuma gari aina ya Scania yenye namba za usajili T.944 AWB na tela lenye namba za usajili T.664 BSJ iliyokuwa ikiendeshwa na Shabani Omary (28) ambapo gari hilo kubwa lilikuwa limeegeshwa barabarani kwa sababu lilikuwa limeharibika.

Aidha Kamanda alisema mtu mmoja jina Mwajuma Kimota (60) alifariki dunia akiwa hospitali ya Mafinga anaendelea na matibabu baada ya kugongwa na pikipiki.

Kamanda alisema tukio hilo lilitokea mnamo tarehe 1 machi majira ya saa 2 kamili usiku katika kijiji cha Makongo, tarafa ya Ifwagi wilaya ya Mufindi hata hivyo dereva na namba za usajili za pikipiki hiyo hazikutambuliwa ambapo dereva alikimbia mara baada ya ajali kutokea.

Mbali na matukio hayo ya vifo Kamanda Mungi alisema JESHI la polisi linamshikilia Riziki Mgatabanhu (19) mfanyabiashara wa Ipogoro kwa kosa la kukutwa na bhangi kete 38 akiwa amezihifadhi kwenye mfuko wa rambo.
Kamanda alisema tukio hilo lilitokea mnamo tarehe 2 machi majira ya saa 3:45 wakati askari polisi wakiwa doria na kusema mtuhumiwa ni muuzaji wa biashara hiyo.
MWANDISHI , DIANA BISANGAO WA MATUKIO DAIMA.COM, IRINGA

KICHANGA CHA MIEZI 6 CHATUPWA KICHAKANI HUKO KAHAMA

Maiti ya mtoto huyo
Mtoto wa kiume anayekadiriwa kuwa na miezi 6 ambaye hajatambulika jina lake wala makazi amekutwa amefariki dunia kichakani baada ya kutupwa na mtu asiyefahamika katika kijiji cha Mhongolo wilayani Kahama
Afisa Mtendaji wa Kijiji hicho Ally Manyama amesema kuwa  baada ya kufika eneo la tukio alikuta mwili wa mtoto huyo ukiwa umeviringishwa katika kitenge na kutupwa kichakani katika eneo hilo.
Jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga limethibitisha kutokea kwa tukio hilo