Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Saturday, December 13, 2014

PICHA::AKUTWA AMEJINYONGA PORINI MKOANI TANGA



Sehemu ya Wananchi wakazi wa Mji wa Pongwe Mkoani Tanga wakiangalia mwili wa mtu huyo uliokuwa ukining'inia juu ya mti.Ambapo mpaka ripota wetu anaondoka eneo la tukio hakukuwa na Mwanausalama yeyote aliefika eneo hilo.
Wakazi wa Mji wa Pongwe wakiuangalia mji huo kwa masikitiko makubwa.


PICHA 5 ZA WEMA SEPETU AKIWA NCHINI GHANA

 Wema Sepetu star wa filamu Tanzania yupo nchini Ghana akifanya kitu wanachokipa Jina PROJECT Na msanii Van Vicker na hizi ni baadhi ya picha alizoweza kushare nasi na caption zake..::
Wema Sepetu na Van Vicker
"In the Making.... @iam_vanvicker @iam_vanvicker@iam_vanvicker"
 Wema Sepetu na Van Vicker"Day 3... & Im loving Ghana already..... ������ Silly us before we start shooting our next scene.... #NextBigThing#DayAfterDeath (D.A.D) starring Myself and Ghana's very own Van Vicker @iam_vanvicker ....@iam_vanvicker @iam_vanvicker @iam_vanvicker@iam_vanvicker .... Let me nat forget he is also Directing it ey...."

MFANYABIASHARA AJIUWA KWA KUJIPIGA RISASI

MWEZI mmoja baada ya mfanyabiashara wa Arusha, Timoth Mroki (36) kujiua kwa kujipiga risasi, mfanyabiashara mwingine maarufu wa Moshi, Augustino Mallya, naye amejiua kwa kujipiga risasi akiwa nyumbani kwake Anakoishi eneo la mtaa wa MAGEREZA KARANGA katika Manispaa ya Moshi.
 Mfanyabiashara huyo alikuwa akijishughulisha na biashara za maduka ya bidhaa za jumla na nyumba

Wakuu wa Mkoa wamtembelea na kumjulia hali Rais Kikwete

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wakuu wa mikoa waliowawakilisha wenzao kwenda ikulu leo kumjulia hali na kumpa pole kufuatia upasuaji alifanyiwa mwezi uliopita nchini Marekani.(picha na Freddy Maro)

DIAMOND NA OMMY DIMPOZ KUWANIA TUZO ZA HMA UGANDA 2015


Ommy Dimpoz na Diamond wakipeana mkono wa kheri.
Nyota wa muziki wa kizazi kipya nchini Tanzania, Diamond Platinum na Ommy Dimpoz wametajwa kuwania tuzo za muziki za nchini Uganda ziitwazo HiPipo Music Awards (HMA) 2015 zinazotarajiwa kutolewa rasmi February 07, 2015.
 Diamond na Dimpoz watachuana katika kipengele kimoja cha ‘East Africa Super Hit’ kupitia nymbo zao Ndagushima na Number One original.
 Katika kipengele hicho wakali hao watachuana na Sauti Sol, Jaguar, Eddy Kenzo, Baramushaka, Urban Boys na Bebe Cool.

MSICHANA WA KAZI ALIYETESA MTOTO AKIRI MAKOSA, KUHUKUMIWA JUMATANO DESEMBA 11, 2014

Msichana wa kazi aliyetikisa vyombo vya habari duniani kwa kumtesa mtoto wa miezi 18, Arnella Kamanz aliyekuwa kwenye uangalizi wake huko Uganda, amekiri makosa mbele ya mahaka nchini humo.
Jolly Tumuhiirwe, mwenye umri wa miaka 22, alifanya ukatili uliochukiwa na watu wote Duniani, ambapo alinaswa na camera ya siri, akimtandika mtoto wa mdosi wake kwa kumkanyaga mgongoni akiwa ameanguka chini, kumchapa na kitu kisichojulikana na kumpiga mateke na makofi ya nguvu usoni.
Kitendo hicho kilifuatia mtoto huyo wa kike, kushindwa kula, kutokana na kasi ya ulishwaji ambapo Tumuhiirwe, alikuwa akimlisha mtoto huyo kwa kasi ya ajabu, kwa kushindilia vijiko mdomoni mfululizo.

Huenda mahakama hiyo ikamuhukumu kifungo cha hadi miaka 15 jela, kulipa faini au vyote kwa pamoja. Msichana huyo katika maelezo yake mahakamani, aliomba radhi wazazi wa mtoto huyo, taifa la uganda na walimwengu wote waliokereka na kitendo chake na kuomba msamaha. Hukumu yake itatolewa Jumatano Desemba 11, 2014.

Hata hivyo wakili wa msichana huyo wa kazi aliyekiri kosa hilo Desemba 8, 2014, amedai kuwa mteja wake hakutendewa haki kwa vile hakuelewa mashtaka yaliyokuwa yakimkabili.

Arnella Kamanzi, binti mrembo na mcheshi mwenye umri wa miezi 18 tu, aliyeteswa na Tumuhiirwe

Nguo hizi za ndani zinasemekana kuwa na uwezo wa kulinda wanaume kutokana na madini hatari yanayoathiri nguvu za kiume

 Nguo hizi za ndani zinasemekana kuwa na uwezo wa kulinda wanaume kutokana na madini hatari yanayoathiri nguvu za kiume
Kampuni ya Belly Armor, ambayo ilikua ya kwanza kutengeza bidhaa zinazohitajika na wanawake wajawazito, kutokana na kitambaa maalum kinacholinda mwili kutokana na athari za madini ya chuma mwilini, imeanzisha biasharta nyingioenkwa manufaa ya wanaume.

Kampuni hii imeanza kutengeza nguo za ndani za wanaume ambao zinawalinda kutokana na athari ya madini ya chuma yanayoweza kupunguza nguvu za kiume na kuathiri uzalishaji wa mbegu za kiume hali ambayo inaweza kusababisha mwanaume kukosa kuzalisha.
Unaweza kujiuliza je biashara ya kutengeza vitambaa hivyo inanawiri? Jibu? Ndio tena sana.
Mbegu za wanaume zinaweza kuthiriwa na madini yanayotumiwa kutengeza simu za mkononi
Mnamo mwaka 2011, shirika la afya duniani lilitaja madini hayo hatari ikiwemo miale inayotokana na simu za mkononi kama yenye uwezo wa kusababisha saratani ya ubongo mbali na athari nyinginezo hatari kwa mwili kiafya.
Kwa mfano, watumjai wa Iphone, je mlijua kama mnapaswa kuzibeba simu zenu umbali wa milimita 10 kutoka kwa mwili wako kuhakikisha kuwa madini hayo hayaathiri mwili?

WAZAZI WA MISS TANZANIA 2O13 WAELEKEA LONDON KUMPA SAOTI MTOTO WAO

 Wazazi wa Miss Tanzania 2O13  Happiness Watimanywa  Akiongozwa na Baba yake wa Tatu Kutoka Kushoto Pamoja na Mama yake wa Tatu Kutoka Kulia WakiwaWameambatana na Wadogo wa Miss Tanzania 2O13 Pamoja na Marafiki Wengine Wakiwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere Katika Hatua za Mwisho Kabla ya Kusafiri Mchana wa Leo Kuelekea Jijini London Kwenye Kilele cha  Mashindano ya Miss World 2O14 Yakakayohitimishwa Tarehe 14.12.2O14  Ambapo Mtoto wao Miss Tanzania 2O13  Happiness Watimanywa Anaiwakilisha Tanzania.

 Wazazi Hao wa  Miss Tanzania 2O13  Happiness Watimanywa  Wamewaomba  Watanzania Kumwombea NA Kuendelea Kumpigia Kura Miss Tanzania 2O13 Katika Mashindano Hayo Ili Aweze Kuiwakilisha Tanzania Vema na Kuibuka Mshindi.Ikumbukwe Mpaka Juzi Miss Tanzania 2O13  Happiness Watimanywa Kura za Watanzania Zilimuwesha Kuingia Kumi Bora.

Ingia humu kufata maelezo ya Namna ya kumpigia kura…..
NA MATUKIO TZ BLOG


AJALI YAUA WATATU BUNJU

Gari aina ya Toyota VX likiwaka moto baada ya kuchomwa na wananchi  Bunju B jijini Dar kwa kusababisha ajali na kuuwa madereva watatu wa bodaboda.
Wananchi wakiwa eneo la tukio baada ya gari aina ya Toyota VX imeua madereva watatu wa bodaboda 
... Gari Likiendelea kuteketea kwa moto.
GARI aina ya Toyota VX imeua madereva watatu wa bodaboda Bunju B, Dar na gari hiyo kuchomwa moto na wananchi

CCM YAWASAMBARATISHA UKAWA UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA, YAZOA MAELFU

Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akisalimiana na baadhi ya viongozi wa CCM baada ya kuwasili katika mkutano wa kufunga kampeni za Uchaguzi wa serikali za Mitaa za Jimbo la Ilala, Dar es Salaam, leo jioni
Wana CCM wakimshangilia Nape alipowasili kwenye mkutano huo
Wananchi wakimshangilia Nape alipowasili kwenye mkutano huo
Nape akiwa Jukwaa Kuu pamoja na viongozi wa CCM baada ya kuwasili kwenye mkutano huo

TANZANIA YASAINI MKATABA WA SH. BILIONI 15.5 KUTOKA BENKI YA ADB KUBORESHA KITUO CHA UTAFITI MUHAS.


Katibu Mkuu Wizara ya fedha Bw. Servacius Likwalile (kushoto) akisaini Mkataba wa mkopo wenye masharti nafuu kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika (ADB) kwa ajili ya kuboresha kituo cha utafiti wa magonjwa ya moyo kinachosimamiwa na Chuo Kuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS)  jijini Dar es salaam. Kulia ni Muwakilishi wa Benki ya ADB nchini Tonia Kandiero akisaini mkataba huo kwa niaba ya Rais wa benki hiyo Dkt. Donald Kaberuka. 


Katibu Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Donan Mmbando (kushoto) akitoa neno la shukurani baada ya kusainiwa  Mkataba wa mkopo wenye masharti nafuu kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika (ADB) kwa ajili ya kuboresha kituo cha utafiti wa magonjwa ya moyo kinachosimamiwa na Chuo Kuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS)  jijini Dar es salaam. Wa kwanza kulia ni Muwakilishi wa Benki ya ADB nchini Tonia Kandiero na katikati ni Katibu Mkuu Wizara ya fedha Bw. Servacius Likwalile. 




 Katibu Mkuu Wizara ya fedha Bw. Servacius Likwalile (kushoto) akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es salaam wakati wa kusaini Mkataba wa mkopo wenye masharti nafuu kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika (ADB) kwa ajili ya kuboresha kituo cha utafiti wa magonjwa ya moyo kinachosimamiwa na Chuo Kuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS).

(Picha zote na Eleuteri Mangi – MAELEZO).

FILAMU MBILI ZA PROIN PROMOTIONS ZAINGIA KWENYE KINYANG'ANYIRO CHA TUZO ZA AFRICA MAGIC VIEWERS CHOICE AWARD‏

Two Tanzanian movies Mdundiko and Network have been nominated for Nigeria Awards, the 2015 Africa Magic Viewers Choice Awards which will take place early next year. Both movies are nominated in the category of  Best Indigenous Language – Swahili and they are competing with Kenyan films. Mdundiko which is directed by Timoth Conrad stars Lumolwe Matovolwa, Dokii,Tino, Rado, Masinde and Bi. Mwenda while Network directed by John Kalaghe stars Monalisa Yvonne Cherryl in the lead.
Jinsi ya Kupiga Kura Unachotakiwa kufanya ni kufungua website hii www.amvca2015-awards.dstv.com and start voting! Unaweza kupiga kura mpaka 100 kwa Siku na vilevile unaweza kupiga kura kwa Kutuma Sms mpaka 100 pia kwa Siku pindi Tuzo hizo zitakapoanza
Vilevile Unaweza kupiga kura kwa kutumia program iitwa WE CHAT ambapo utatakiwa kuidownload kwenye simu yako na kuanza kupiga kura

DIWANI MATHIUS WA KATA YA MALANGARINI AFUNGA KAMPENI ZA UCHAGUZI KATANI KWAKE‏


Diwani wa kata ya Mlangarini, Mathius Manga akizungumza na wananchi wa kata hiyo katika mkutano wa hadhara wa kuhitimisha kampeni za uchaguzi wa CCM kwa ajili ya kuwachagua viongozi wa  serikali za mitaa utakaofanyika jumapili Desemba 14 mwaka huu.

Diwani Manga amewaasa wananchi wote kujitokeza kwa wingi kuwapigia kura wagombea wa CCM kwani wanasifa stahiki za kuwaongoza. 

Aidha amesisitiza kulimnda amani kipindi cote cha uchaguzi na hata matokeo yatakapo tangazwa na kuepuka vitendo vya vurugu. 
 Wananchi wa kata ya Manyire wakimsikiliza diwani wa kata hiyo hayupo pichani wakati wa kuhitimisha kampeni za uchaguzi wa serukali za mitaa.

MDAU ANGELA AKILIMALI NA WENZAKE WALA NONDO YA MAWASILIANO YA UMMA

Kaimu Mgukurugeni wa Uhuru FM, Angela Akilimali (katikati) akiwa na wahitimu wenzake wa Shahada ya Mawasiliano ya uma ya Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT) katika mahafali yaliyofanyika hivi katibuni mkoani Kibaha mkoani Pwani.  Kushoto ni Hemed Mbaraka na Mganwa Nzota.
 Wanahabari wa morogoro nao walikula nondo zao katika mahafali hayo.