Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Friday, March 27, 2015

Baba mbaroni kwa kuwabaka watoto wake

Rahma Mashamu ambaye ni mama mzazi wa watoto wawili mmoja wa miaka 11 na mwingine 15 wanaodaiwa kubakwa na baba wa watoto hao akilia kwa uchungu wakati akihojiwa na waandishi wa habari kuhusiana na tukio hilo, wilayani Kibaha mkoani Pwani. Picha na Julieth Ngarabali 


Simulizi za watoto
 Wakizungumza nyumbani kwao jana watoto hao, walisema baba yao alikuwa akiwatishia kuwakatakata kwa panga au kuwakaba koo humohumo chumbani endapo wangethubutu kumweleza mtu yeyote kitendo wanachokifanya.
 “Tulikuwa tumeingia kwetu kulala na wadogo zangu, nikasikia ananiita nikambembeleze mtoto eti anamsumbua, nilikwenda nikambembeleza  akalala, 
 
wakati nashuka kitandani kurudi chumbani kwetu baba akanivuta kwake akanivua, akasema anachokifanya ni suna kwa hiyo hataki kelele, akisikia atanikaba nife.”

“Niliumia sana na asubuhi mama alirudi nikajitahidi kweli asijue na hata shule sikwenda, jioni mama aliondoka tena baba hakuniita siku hiyo lakini baada ya siku tatu aliniita tena ikawa vilevile navumilia. Siku zilivyozidi unaweza kukuta kwa wiki naitwa hata mara nne siku ambazo mama hayupo nyumbani,” alisema.

Watoto hao walieleza kuwa baadaye baba huyo alihamia kwa binti mdogo kwa staili ileile na kila mmoja alikuwa akiitwa kwa zamu na kwa vile kila mmoja alijua ni siri yake na baba. Kutonaka na woga wa kuuawa, hakuna aliyemweleza mwenzake hadi katikati ya mwaka jana mmoja wao alipomweleza mwenzake na baadaye kumweleza mama yao.

“Baba alikuwa anasema atatuua bila hata mtu kujua na tutaozea shambani, hata nikiwa katika siku zangu baba ananiingilia hivyohivyo, naugua kila mara UTI, mdogo wangu naye kila mara UTI, tukaamua liwalo na liwe kama kufa basi ila mama ajue,” alisema mtoto huyo huku akibubujikwa na machozi.

Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Miembe Saba, Hamis Shomari alisema kabla ya kupelekwa kituo cha polisi Kongowe Jumamosi iliyopita, watoto hao waliitwa shuleni hapo na kuhojiwa kila mmoja peke yake na wote walikiri kuanza kubakwa mwaka 2013 na baba yao na kwamba tabia hiyo iliendelea hadi Machi 19 usiku alipobakwa binti mdogo kwa mara ya mwisho na Machi 20 walipoamua kumweleza mama yao.

 Kamanda wa Polisi mkoani Pwani, Ulrich Matei alisema wanamshikilia mtuhumiwa huyo na kwamba wasichana hao wamefanyiwa vipimo mbalimbali na majibu ya daktari yamethibitisha kuwa wamebakwa na sehemu zao za siri  zimeharibiwa, hivyo wanaendelea na matibabu.

No comments:

Post a Comment