

Mlipuko mkubwa uliotokea katika mji wa Tianjin kaskazini mwa China umeuwa watu 50 huku wengine wapatao 700 wakijeruhiwa.

Moshi mweusi bado umetanda kutoka ghala hilo lililopo katika mji wa bandari wa Tianjin ambako milipuko ilitokea jana usiku.

Mabweni ya wahamiaji yaliporomoka kutokana na milipuko hiyo.

Video zilizowekwa katika mitandao ya kijamii zinaonyesha moto mkubwa na wingu kubwa la moshi lililotanda angani.

Mlipuko huo mkubwa katika mji wa China Tianjin-ambao ni mji wa Bandari kuu na sehemu ya viwanda katika eneo la kusini kaskazini mwa mji mkuu Beijing unadaiwa kuwajeruhi mamia ya watu ingawa kufikia sasa idadi kamili haijulikani.

Shirika la habari la nchi hiyo, Xinhua limesema mlipuko huo ulisababishwa na kemikali zilizokuwa zimehifadhiwa katika bohari moja katika bandari hiyo.

CHANZO: BBC SWAHILI
No comments:
Post a Comment