Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Saturday, October 31, 2015

Obama aing'oa Burundi kutoka kwenye AGOA


Marekani imeiondoa Burundi kutoka kwenye mikataba yake ya kibiashara AGOA iliyowezesha mataifa ya Afrika kuingiza bidhaa zao katika soko la Marekani bila kulipa kodi.
Marekani imeiondoa Burundi kutoka kwenye mikataba yake ya kibiashara AGOA iliyowezesha mataifa ya Afrika kuingiza bidhaa zao katika soko la Marekani bila kulipa kodi.Katika barua aliyoiandikia bunge la Congress , rais Barrack Obama ameelezea kuwa amechukua hatua hiyo baada ya kushuhudia kushuka kwa viwango vya demokrasia katika taifa hilo la Afrika ya Kati.
''Burundi haijafanya jitihada zozote za kurejesha amani na utangamano'' Obama.
''Burundi haijafanya jitihada zozote za kurejesha amani na utangamano'' Obama.

 
Obama alisema kuwa badala ya kuimarika kidemokrasia, Burundi inaendelea kushuhudia wapiganiaji wa haki za kidemokrasia wakikamatwa na kufungwa jela huku wengine wengi wakiuawa kwa kudai haki zao za kikatiba zifwatwe.
Aidha Obama ameelezea kuwa hatua ya serikali ya rais Nkurunziza ya kuwanyamazisha makundi ya wapinzani kwa kuwashika kuwaua na hata kuwatesa ni kinyume na maadili ya taifa linalodai kuzingatia demokrasia.
Image copyrightReuters
Image captionTakriban watu 200 wameuaawa tangu machafuko yaanze mwezi Aprili
Marufuku hiyo ya Burundi inaanza kutekelezwa mwezi januari mwakani.
Burundi ilitumbukia katika mzozo wa kisiasa na kukumbwa na machafuko punde baada ya rais Pierre Nkurunziza kutangaza nia ya kuwania muhula wa tatu kinyume na katiba ya taifa.
Aidha kulitokea jaribio la mapinduzi lakini likazimwa.
Image copyrightAFP
Image captionTakriban watu 200 wameuaawa tangu machafuko yaanze mwezi Aprili upinzani ulipopinga hatua ya Nkurunziza kushiriki kwenye uchaguzi kwa muhula wa tatu.
Nkurunziza alishiriki uchaguzi huo na akashinda, hata hivyo kumeendelea kuwa na visa vya maandamano,mauaji na kutoweka kwa wapinzani wake.
Takriban watu 200 wameuaawa tangu machafuko yaanze mwezi Aprili
Inakisiwa kuwa watu 200,000 wametoroka makwao na sasa wanaishi kwenye kambi za wakimbizi katika mataifa jirani.
Mpango wa AGOA (African Growth and Opportunity Act) ulianzishwa yapata muongo mmoja uliopita ilikuzisaidia mataifa maskini ya Afrika kuuza bidhaa zao katika soko la Marekani.Chanzo BBC Swahili

No comments:

Post a Comment