Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Sunday, November 1, 2015

WATU 6 WAFARIKI KATIKA AJALI YA BARABARANI MOROGORO


Watu sita wamefariki dunia baada ya gari ndogo waliokuwa wakisafiria kugongana uso kwa uso na basi la abiria mali ya kampuni ya Princess Muro, lililokuwa likitokea Dar es salaam kuelekea Tunduma, katika eneo la hifadhi ya taifa ya Mikumi, barabara kuu ya Morogoro-Iringa.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro Leonard Paulo amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo katika eneo la hifadhi ya taifa ya Mikumi, ikihusisha gari ndogo la abiria aina ya Toyota Noah lenye namba za usajili T 359 BBA iliyokuwa imebeba abiria sita wakiwemo wanawake wawili na wanaume wanne ambayo ilipasuka tairi ya Mbele ya kuyumba ovyo barabarani na kugongana na basi hilo la Princess Muro lenye namba T 160 BBC na kusababisha vifo kwa abiria wote wa Noah.

No comments:

Post a Comment