Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Wednesday, December 2, 2015

DKT. SLAA ATOA TATHMINI YA MAAMUZI YA RAIS MAGUFUL


Aliyekuwa katibu Mkuu wa Chadema, Dkt. Wilbroad Slaa ametoa tathmini yake kwa siku chache za Rais John Magufuli alizoanza kazi katika Serikali ya Awamu ya Tano na maamuzi aliyoyafanya.
Dkt. Slaa ambaye alikuwa mgombea urais kupitia Chadema mwaka 2010, ameeleza kuwa maamuzi ya kufuta safari za nje kwa watendaji wa serikali yaliwahi kuchukuliwa na Rais wa Serikali ya Awamu ya kwanza, Mwalimu Julius Nyerere.
Alisema kuwa hata wapinzani walikuwa wakilalamikia gharama zinazotumika kwenye safari za nje na kwamba yeye pia aliwahi kupendekeza safari hizo kufutwa na badala yake watendaji waende vijijini kuchagiza maendeleo.
“Tulilamikia safari za JK nje ya nchi. Na mimi niliwahi kusema kuwa tufute 


 
safari za njena kuanza kwenda zaidi vijijini. Tuone naye kama katufa tu… na badala yake tufanye nini. Ni siku mbili (Jumamosi) ofisini huwezi kufanya tathmini ya maana,” alisema.
“Tathmini hii kwa kawaida hufanywa baada ya siku 100. Mwalimu alifanya hivyo. Rais wa watu ni vyema akifanya hivyo. Ndiyo namna pekee ya kujua hali halisi. Kwa Magufuli si ya kwanza, amefanya sana akiwa Waziri.”
Mpekuzi blog

No comments:

Post a Comment