Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Sunday, December 29, 2013

Baada ya Kutimuliwa Uwaziri: Shamsi aungana na wazanzibari wanaotaka Mamlaka Kamili ya nchi yao.?Soma maneno yake hapa





Mwakilishi wa jimbo la Mwanakwerekwe Shamsi Vuai Nahodha amesena anaungana na kundi la wazanzibar wanaotaka Zanzibar kuwa na mamlaka kamili ndani ya katiba ijayo ya Jamhuri ya muungano Tanzania.

Akizungumza na wanachama na viongozi katika ofisi za CCM mkoa wa Mjini (kichama) amesema katika baadhi ya maeneo ya kuendesha nchi suala la mamlaka kamili ni muhimu kuimarisha uchumi wa Zanzibar.

Nahodha aliewahi kuwa waziri wa mambo ya ndani na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa amedai yeye ni mtetezi wa suala la mafuta na gesi liondolewe kwenye muungano.

Hata hivyo amesema anashangazwa na baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa wanaodai sarafu ya Zanzibar, kiti cha umoja wa mataifa na wizara ya ulinzi akidai masuala hayo yanahitaji gharama kubwa za uendeshaji.

Aidha Nahodha amesema wakati Zanzibar ikiendelea kuadhimisha miaka 50 ya Mapinduzi Zanzibar muungano utaendelea kubaki uti wa mgongo wa maendeleo ya ulinzi na usalama wake.

Amesema licha ya mfumo wa muungano wa serikali mbili kujaa matatizo, lakini njia ya kuyapatia ufumbuzi ni Zanzibar huru badala ya kung'ang'ania muungano wa mkataba au serikali tatu.

TUNAOMBA BOFYA HAPA NA ULIKE PAGE YETU KWA HABARI NYINGI ZA KILA SIKU,(USIPITWEEEEEEEE)

No comments:

Post a Comment