Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Sunday, April 13, 2014

CDA MABINGWA WAPYA WA MKOA WA DODOMA

 Mchezaji wa timu ya CDA Dotto Maheche akipiga mpira kuelekezwa katika lango la Gunnars huku Shaff Kanuani akijaribu kumkaba, katika mchezo wa mwisho uliokuwapa CDA ubingwa mkoa baada ya kutoka suluhu ya bila kufungana.
 Aron Michael Wa CDA akimilki mpira mbele ya wachezaji wa Gunnars ambapo mchezo huo ulimfanya bingwa kuibuka bingwa wa mkoa wa Dodoma baada ya kufikisha jumla ya pointi 13 zidi ya 10 za Gunnars.



Mashabiki wa timu zote mbili wakishangilia kwa wakati mchezo huo ulipokuwa ukiendelea ambapo kila timu ilikuwa ikisaka ushindi ili kuibuka bingwa.

 Na John Banda, Dodoma
TIMU ya CDA iliyopata kuwika miaka ya nyuka katika ligi kuu ya Vodacom imefanikiwa kunyakua ubingwa wa Mkoa wa Dodoma hivyo kufuzu kushiriki ligi ya mabingwa wa mkoa  itakayofanyika baadae mwaka huu. CDA walipata ubingwa huo kwa mbinde baada ya kulazimishwa Suluhu ya bila kufungana na timu ngumu ya wanajeshi wa ihumwa Gunnars baada ya kubanana vilivyo katika vipindi vyote katika uwanja wa jamhuri juzi.
Timu hiyo ya watoto wa nyumbani iliucheza mchezo huo huku ikiwa inahitaji sale ili ifuzu huku Gannars wakilazimika kushinda ili kuipiku pointi moja ktokana wao kua na pointi 10 wakati mabingwa hao
wakiwa na 12.
Baada ya mchezo huo kocha wa timu hiyo Juma Ikaba alisema walikuwa na safari ngumu kutokana na kila timu waliyokutana nayo ilikuwa inawakamia, lakini akawapongeza vijana wake kwa kujituma. Ikaba aliwataka wanadodoma kujua kuwa timu hiyo ni ya kwao hivyo wanatakiwa kushikamana bega kwa bega ili kuiwezesha iweze kuvuka na hatua zinazofuata ikiwemo bingwa wa mikoa na baadae ipande ligi kuu.
Aidha alisema imefika wakati wananchi wa mkoa huu kushikamana vilivyo ili kuhakikisha timu hiyo inapanda ligi kuu tofauti na kipindi cha nyuma ambacho timu hiyo ilipokuwa ikipanda watu walikuwa wanaiacha kiasi cha kujiona ni yatima mkoani kwao.
Jumla ya mechezo kumi na tano imechezwa iliyozikutanisha jumla ya timu sita za Sheli, vijana Chamwino, Area C, Kikuyu, Gunnas na Mabingwa hao waliyowahi kushiriki Michuano ya Africa mashariki na kati miaka ya 90, huku Mashabiki wa mchezo huo wakiwa na shauku ya kuziona timu za ligi
kuu zikitia maguu katika uwanja wa jamhuri kama ilivyokuwa miaka ya nyuma.

No comments:

Post a Comment